Pata taarifa kuu

UNICEF: Watoto 289 walifariki wakivuka bahari ya Mediterania mnamo 2023

Takwimu hizo ni za kutisha na zinaongezeka kwa kasi, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na kuhudumia watoto, UNICEF. Hiyo ni wastani wa watoto kumi na moja wanaokufa kila wiki.

Wahamiaji wanasubiri kuokolewa na Walinzi wa Pwani ya Italia kwenye pwani ya Italia, Aprili 10, 2023.
Wahamiaji wanasubiri kuokolewa na Walinzi wa Pwani ya Italia kwenye pwani ya Italia, Aprili 10, 2023. © Italian Coast Guard / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Takriban watoto 289 tayari wamefariki mwaka huu wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania kufika Ulaya. UNICEF ​​​​inatoa tahadhari: idadi ya watoto ambao wamepoteza maisha wakati wakivuka bahari ya Mediterania imeongezeka mara mbili ikilinganishwa na mwaka jana.

Kulingana na Verena Knaus, mkuu wa mpango wa uhamiaji wa UNICEF, sababu kadhaa zinaelezea mwelekeo huu wa kuongezeka kwa idadi hiyo. “Kutokana na mizozo ya Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Afŕika Maghaŕibi, lakini pia nchini Afghanistan, na madhaŕa ya hali ya hewa na hataŕi za hali ya hewa, kuanzia ukame hadi mawimbi ya joto, watoto zaidi na zaidi wanalazimika kuondoka majumbani mwao. Na watoto zaidi na zaidi wanalazimika kufanya safari hizi za hatari kubwa kuvuka bahari hadi kufikia Ulaya ", Verena Knaus ameongeza.

Watoto wengi husafiri peke yao

Kwa mujibu wa UNICEF, zaidi ya watoto 11,000 wamevuka bahari ya Mediterania tangu mwanzoni mwa mwaka huu, mara mbili zaidi ya mwaka jana. Na wengi wao walikuwa wakisafiri peke yao. “Watoto wanakufa kwa sababu hakuna njia salama zisizo halali. Watoto wanakufa kwa sababu hakuna uwezo mkubwa wa utafutaji na uokoaji uliowekwa ili kuzuia vifo hivi,” Verena Kraus amebainisha. Anashutumu jumuiya ya kimataifa kwa kustahimili hatari mbaya zinazohusiana na uhamiaji wa watoto. "Wanakufa na tunaamua kufumba macho," amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.