Pata taarifa kuu
MAZUNGUMZO-AMANI

Mjumbe wa Papa azuru Moscow kujaribu kufanya mazungumzo ya amani nchini Ukraine

Wiki tatu baada ya kuzuru Kyiv, mjumbe wa kiongozi wa kanisa Katolika Papa Francis wakati huu yuko nchini Urusi. Kadinali wa Italia Matteo Zuppi yuko Moscow leo Jumatano Juni 28 na kesho Alhamisi Juni 29 kukutana na viongozi wa Urusi. Kazi ngumu kwa Vatican na Papa Francis ambaye bado anaamini katika kuna uwezekano wa kujadili amani.

Kardinali Matteo Zuppi, hapa wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Vatican tarehe 25 Mei, 2023.
Kardinali Matteo Zuppi, hapa wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Vatican tarehe 25 Mei, 2023. © Domenico Stinellis / AP
Matangazo ya kibiashara

Ni kazi ngumu, ambayo Kadinali Zuppi atatekeleza katika mji mkuu wa Urusi, anaripoti mwandishi wetu wa Vatican, Éric Sénanque.

Askofu Mkuu wa Italia atazungumza na Kirill 1st, kiongozi wa kiroho wa Kanisa la Urusi na ambaye anaunga mkono vita nchini Ukraine. Mkutano huo ambao umetajwa na vyombo vya habari vya Urusi, haujathibitishwa.

Wakati wa ziara yake mjini Moscow, mjumbe wa papa anatarajiwa kukutana na mshauri wa sera za kigeni wa Kremlin Yuri Uchakov siku ya Alhamisi. Suala la jukumu la Vatican katika kubadilishana wafungwa litakuwa kwenye ajenda ya majadiliano.

Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, Kremlin inasalimu "juhudi" za Vatikani. "Watazungumza juu ya mzozo wa Ukraine na uwezekano wa suluhu ya amani," msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema juu ya mkutano na afisa wa Moscow, akiongeza kwamba Kremlin "inathamini sana juhudi na mipango ya Vatican kupata suluhisho la amani. kwa mgogoro wa Ukraine".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.