Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Kakhovka: Nchi za Magharibi zashutumu Urusi kwa 'kitendo cha kashfa' na 'uhalifu wa kivita'

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema Jumanne Juni 6 kwamba alikasirishwa na shambulio kwenye bwawa la kuzalisha umeme la Kakhovka, ambalo "linaonyesha kwa mara nyingine ukatili wa vita vilivyoanzishwa na Urusi".

Bwawa la kuzalisha umeme la Kakhova, Juni 6, 2023.
Bwawa la kuzalisha umeme la Kakhova, Juni 6, 2023. AP
Matangazo ya kibiashara

Uharibifu wa bwawa la Kakhovka ni "kitendo cha kashfa" ambacho "huhatarisha maelfu ya raia na kusababisha uharibifu mkubwa kwa mazingira", ameandika Jens Stoltenberg. Hapo awali, Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel alisema Urusi inapaswa kuwajibika. 

"Nimeshtushwa na shambulio ambalo halijawahi kutokea kwenye bwawa la Nova Kakhovka," aliandika Charles Michel. "Uharibifu wa miundombinu ya kiraia ni uhalifu wa kivita na tutawajibisha Urusi na washirika wake." 

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema katika mahojiano na WDR na ZDF kwamba shambulio hilo limeipa vita vya Urusi dhidi ya Ukraine "mwelekeo mpya", "lakini ambayo pia inalingana na jinsi Putin anavyoendesha vita hivi". "Pia ni jambo ambalo ni sehemu ya uhalifu mwingi ambao tumeona nchini Ukraine, ambao ulifanywa na wanajeshi wa Urusi na ni sehemu ya njia ya vita ambayo imekuwa ikilenga raia - miji, vijiji, hospitali, shule, miundombinu,” kiongozi huyo wa Ujerumani amesema. Kwa upande wake, Uingereza pia imeshutumu shambulio la Kakhovka. "Uharibifu wa bwawa la Kakhovka ni kitendo kibaya, ameandika mkuu wa diplomasia, James Cleverly. Shambulio la kukusudia kwa miundombinu ya kiraia pekee ni uhalifu wa kivita. Uingereza iko tayari kusaidia Ukraine na watu walioathiriwa na janga hili. "

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.