Pata taarifa kuu

Washirika wa Ukraine hawatasambaratika: Waziri wa ulinzi wa Marekani

NAIROBI – Marekani imeandaa mkutano nchini Ujerumani kujadili uungaji mkono zaidi kwa Ukraine baada ya rais Volodymyr Zelensky kuwasukuma washirika wa Magharibi kutuma ndege zaidi za kivita na makombora ya masafa marefu.

Mawaziri wa ulinzi wa nchi za NATO
Mawaziri wa ulinzi wa nchi za NATO © Matthias Schrader / AP
Matangazo ya kibiashara

Wawakilishi kutoka karibu nchi 50 wamekusanyika katika kikao hicho kupanga mikakati zaidi ya uungaji mkono wao kwa Kyiv.

Katika kikao hicho nchini Ujerumani, Lloyd Austin waziri wa ulinzi wa Marekani ameendelea kusisitiza kwamba washirika wa Ukraine wataendelea kuiunga mkono Ukraine baada ya Urusi kuishambulia.

Akizungumza katika mkutano huo, Lloyd Austin aidha amesema kuwa nchi yake iko tayari na imetoa msaada wa thamani ya zaidi ya dola milioni 35 kwa ajili ya msaada wa silaha kwa Ukraine.

Lloyd Austin, Waziri wa ulinzi wa Marekani
Lloyd Austin, Waziri wa ulinzi wa Marekani AP - Matthias Schrader

Vile vile Marekani imeahidi kutoa usaidizi katika kipindi chote cha vita nchini Ukraine, zikiwemo silaha za mafara marefu, na silaha za kuzuia makombora ya kutegwa.

Licha ya Marekani kusistizia suala la kuendelea kuiunga mkono Ukraine, mkuu huyo wa jeshi pia ametumia muda huo kujaribu kurejesha imani na uaminifu kutoka kwa nchi washirika wa marekani baada ya kuvuja kwa nyaraka kuhusu ushiriki wa Marekani katika vita vya Ukraine.

Lloyd amewaeleza washirika wa Washington kuwa nchi yake inawathamini sana na kwamba hawatawahi kugawanyika.

Miongoni mwa usaidizi wa hivi karibuni ni wa silaha za makombora ya masafa aina ya Hymas.

Washirika wa Ukraine wamesisitiza kauli yao ya kuendelea kuisaidia Ukraine
Washirika wa Ukraine wamesisitiza kauli yao ya kuendelea kuisaidia Ukraine © AP - LIBKOS

Urusi kwa upande wake imeendelea kusistiza kauli yake kuwa nchi za Magharibi zimehusika moja kwa moja katika mzozo kati yake na Ukraine baada ya nchi hizo kuaanza kutuma misaada ya kijeshi kuisaidia Ukraine.

Kyiv imekuwa ikitoa wito kwa washirika wake  nchi za Magharibi kuihami na silaha nzito nzito ilikupiga jeki mapambano yake dhidi ya uvamizi wa Moscow.

Kikao hiki kinakuja wakati huu katibu mkuu wa NATO, Jens Stolenburg akifanya ziara nchini Ukraine, ziara yake ya kwanza tangu nchi hiyo kuvamiwa na Urusi.

Akiwa nchini humo, kiongozi huyo wa Nato kwa upande wake amesema kuwa muungano huo utaendelea kutoa msaada pamoja na kusimama na Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.