Pata taarifa kuu

Zelensky: Ukraine iko tayari kukabiliana na mashambulizi, lakini kuna hatari ya kupoteza

Maandalizi ya shambulio la Ukraine yamekamilika, lakini hasara ya maisha inaweza kuwa nzito kutokana na uwezo mkubwa wa jeshi la wanaanga wa Urusi, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky (katikati) baada ya mkutano na waandishi wa habari huko Bulboaca, karibu na Chisinau, Moldova, Alhamisi, Juni 1, 2023. AP - Carl Court.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky (katikati) baada ya mkutano na waandishi wa habari huko Bulboaca, karibu na Chisinau, Moldova, Alhamisi, Juni 1, 2023. AP - Carl Court. AP - Carl Court
Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano yaliyochapishwa Jumamosi hii, Juni 3 na Gazeti la Wall Street, rais wa Ukraine amesema kuhusu shambulio hilo: "Kwa maoni yangu, kuanzia leo tuko tayari (...) Tunaamini kabisa kwamba tutafanikiwa", akibainisha kwamba hajui "itachukua muda gani".

Hata hivyo, ameonya kwamba mashambulizi yatakuwa "hatari" hakutakuwa na  msaada mkubwa wa nchi za Magharibi kukabiliana na mashambulizi ya anga ya Urusi. "Kila mtu anajua kwamba mashambulizi ya kujibu na bila kuwa na uwezo na ubora wa jeshi la wananga ni hatari sana," ameongeza rais wa Ukraine.

  'Hatutaki kuwa mwanachama wa NATO wakati wa vita'

Silaha moja tu, mfumo wa makombora wa Marekani uitwao sol-air américain Patriot, unaweza kulinda anga ya Ukraine, ameongeza, akitoa wito wa kupewa silaha zaidi za aina hiyo kuwasilishwa nchini mwake. "Silaha moja inaipiku Urusi kwa uwezo wake wa kutishia makumi ya mamilioni ya watu: makombora ya Patriots," amesema.

Kwa kuzingatia mkutano wa kilele wa NATO utakaofanyika Vilnius, Lithuania, mwezi ujao, amekiri kuelewa kwamba haiwezekani kwa nchi yake kujiunga na Muungano wa Atlantiki wakati wa uvamizi wa Urusi. "Hatutaki kuwa mwanachama wa NATO wakati wa vita," amehakikisha. "Wakati umepita. Lakini niambie ni watu wa ngapi wanafaa hukumu juu ya Vilnius? »

  "Ikiwa hatutambuliwi na ikiwa hatutapokea ishara huko Vilnius (kwa lengo la uwezekano na uanachama wa baadaye), nadhani ni bure kwa Ukraine kushiriki katika mkutano huu", amebainisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.