Pata taarifa kuu

Nchi za Magharibi zavutana kufuatia ombi la silaha mpya la Ukraine

Ukraine inahitaji silaha mpya ili kukabiliana na hali "ngumu" ya kijeshi mashariki mwa nchi hiyo, Rais Zelensky alisema Jumapili jioni. Jinsi ya kujibu mahitaji haya bila kuweka kidole katika uhasama na Moscow ni kwa nchi za Magharibi kutekeleza yale zilizoaahidi. Kutoka Chile, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amekuwa thabiti: hakuna ndege za kivita kwa Kyiv na huko Seoul, mkuu wa NATO anajifanya kama wakili wa kyiv.

Jimbo la Donetsk, mashariki mwa Ukrainia, tarehe 28 Januari 2023.
Jimbo la Donetsk, mashariki mwa Ukrainia, tarehe 28 Januari 2023. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Ukraine inahitaji silaha mpya na usafirishaji wa haraka wa silaha hizo ili kukabiliana na hali "ngumu" ya mashambulizi ya mara kwa mara ya vikosi vya Urusi katika eneo la mashariki la Donetsk, Rais Zelensky alisema katika ujumbe wa video siku ya Jumapili. Bakhmut, Vougledar na maeneo mengine ya mkoa wa Donetsk yako chini ya "mashambulizi ya mara kwa mara ya Urusi". "Urusi inataka vita viendelee na kuchosha nguvu zetu. Kwa hiyo ni lazima tuwe na muda kwa silaha letu. Tunahitaji kuharakisha matukio, kuharakisha vifaa na kufungua chaguzi mpya za Ukraine kupata silaha za kutosha. "

Suala la uwasilishaji wa silaha kwa Ukraine na asili ya silaha hizi pia liliulizwa kutoka Santiago nchini Chile na Kansela wa Ujerumani, ambaye kwa sasa yuko ziarani Amerika Kusini.

Hakuna ndege za kivita za Berlin

Ujerumani haitatuma ndege za kivita nchini Ukraine, Olaf Scholz alisema Jumapili. Baada ya majuma kadhaa ya kusitasita, Berlin iliamua wiki iliyopita kupeleka vifaru 14 vya Leopard 2 nchini Ukraine, vilivyotengenezwa Ujerumani na kuruhusu nchi nyingine za Ulaya kkuipa Ukraine vifaru hivi . Lakini "Swali la ndege za kivita halijitokezi hata kidogo. Ninaweza tu kushauri dhidi ya kuingia katika vita vya zabuni vya mara kwa mara linapokuja suala la mifumo ya silaha, "alifafanua Chansela katika mahojiano na gazeti la Tagesspiegel, kutoka Santiago.

Uamuzi wa kupeleka vifaru vya Ujerumani nchini Ukraine uliambatana na chaguo sawa na Marekani kulipatia jeshi la Ukraine vifaru vya Abrams vilivyotengenezwa nchini Marekani.

Akizishukuru Berlin na Washington, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliomba mara mojamsaada wa silaha mpya, zikiwemo ndege za kivita na makombora ya masafa marefu. Katika mahojiano yake na Tagesspiegel, Olaf Scholz anaonya tena dhidi ya "hatari ya kuongezeka kwa magigano" na Moscow. "Hakuna vita kati ya NATO na Urusi. Hatutaruhusu vita vya namna hiyo,” alisema.

Olaf Scholz alisema, ni "muhimu" kuendelea kuzungumza na Rais wa Urusi Vladimir Putin. Mazungumzo yao ya mwisho yalifanyika mwanzoni mwa mwezi Desemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.