Pata taarifa kuu
DIPLOMASIA-ULINZI

Ujerumani kupeleka vifaru chapa Leopard Ukraine 'mwisho wa mwezi Machi'

Ujerumani inatarajia kupeleka vifaru aina ya Leopard 2 iliyoahidi Ukraine "mwishoni mwa mwezi Machi, mwanzoni mwa mwezi Aprili". Hivi ndivyo Waziri wa Ulinzi Boris Pistorius amesema siku ya Alhamisi, Januari 26.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akizungumza na wanajeshi mbele ya kifaru chapa Leopard 2 baada ya mazoezi huko Ostenholz, Oktoba 2022.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akizungumza na wanajeshi mbele ya kifaru chapa Leopard 2 baada ya mazoezi huko Ostenholz, Oktoba 2022. AP - Moritz Frankenberg
Matangazo ya kibiashara

"Imepangwa kuwa tutaikabidhio Ukraine vifaru hivyo mwishoni mwa mwezi Machi mwanzoni mwa mwezi Aprili", waziri amesema wakati alipotembelea askari wa Bundeswehr huko Saxony-Anhalt, mashariki mwa nchi.

Mafunzo ya wanajeshi wa Ukraine katika kuendesha vifaru vyepesi vya Marder, vilivyoahidiwa na Berlin mwanzoni mwa mwaka, yataanza "mwishoni mwa mwezi Januari" nchini Ujerumani na mafunzo ya kuendesha vifaru chapa Leopards yatafuata "baadaye kidogo", ameongeza. Ukraine imesema inatumai kupokea vifaru hivi haraka iwezekanavyo.

Baada ya wiki kadhaa Marekani na Ujerumani zikisitasita, nchi hizi mbili zilitangaza Jumatano Januari 25 kukabidhi vifaru vizito kwa Ukraine, na kuchukua hatua mpya katika msaada wa kijeshi kwa Kyiv katika mtazamo wa uwezekano wa kukabiliana na uvamizi wa Urusi.

Poland na Norway zimetangaza kuwa tayari kuipa Ukraine vifaru chapa Leopard 2. Kwa mujibu wa vyombo vya habari kadhaa, muungano wa nchi zilizo tayari kutoa magari hayo ya kivita pia unajumuisha Denmark na Uholanzi, pamoja na Poland na Finland. Uhispania imethibitisha kuwa iko "tayari" kutoa vifaru pia.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.