Pata taarifa kuu

Moscow yadai kuwa wapiganaji 265 wa Ukraine kutoka Azovstal ni wafungwa

Katika siku ya 83 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumanne hii, Mei 17, mashambulizi ya Urusi katika Donbass yameongezeka huko Sievierodonetsk, Mashariki mwa nchi, kituo muhimu cha utawala ambacho bado kiko chini ya udhibiti wa Kyiv.

Wanajeshi wa vikosi vinavyounga mkono Urusi wakati wa zoezi la kuwahamisha wanajeshi wa Ukraine waliojeruhiwa kutoka  kiwanda cha chuma cha Azovstal huko Mariupol, Mei 16, 2022.
Wanajeshi wa vikosi vinavyounga mkono Urusi wakati wa zoezi la kuwahamisha wanajeshi wa Ukraine waliojeruhiwa kutoka kiwanda cha chuma cha Azovstal huko Mariupol, Mei 16, 2022. REUTERS - ALEXANDER ERMOCHENKO
Matangazo ya kibiashara

Kusini mwa nchi, huko Mariupol, operesheni ya uokoaji ya askari ambao bado wamejificha katika kiwanda cha Azovstal bado inaendelea, kulingana na kyiv.

Zaidi ya wapiganaji 260 wa Ukraine, wakiwemo 53 waliojeruhiwa, walihamishwa siku ya Jumatatu kutoka kiwanda cha chuma cha Azovstal, ngome ya mwisho ya upinzani wa Ukraine huko Mariupol, Naibu Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Ganna Malyar, ametangaza. Shughuli ya uokoaji inaendelea Jumanne hii asubuhi.

Mashambulizi ya Urusi katika Donbass yaliongezeka siku ya Jumatatu, na kusababisha watu kumi kupoteza maisha huko Sievierodonetsk, kituo muhimu cha utawala ambacho bado chini ya udhibiti wa kyiv, lakini karibu kuzungukwa na majeshi ya Kirusi.

Sweden itatuma maombi ya kujiunga na NATO, Waziri Mkuu Magdalena Andersson alitangaza rasmi Jumatatu, akirejelea "zama" mpya kwa nchi ya Skandinavia.

Vikosi vya Ukraine vimewatimua wanajeshi wa Urusi na kurejesha udhibiti wa sehemu ya mpaka na Urusi katika eneo la Kharkiv (kaskazini mashariki), mamlaka ya Ukraine ilitangaza siku ya Jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.