Pata taarifa kuu

Urusi: Mkuu wa NATO atoa wito 'kuachiliwa mara moja' kwa mwandishi wa habari wa Marekani

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ametoa wito Jumatatu "kuachiliwa mara moja" kwa mwandishi wa habari wa Marekani Evan Gershkovich, anayezuiliwa tangu siku ya Alhamisi na Urusi, ambayo inamtuhumu kwa ujasusi.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg.
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Kukamatwa kwake kunatia wasiwasi. Ni muhimu kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari, haki za waandishi wa habari, haki ya kuuliza maswali na kufanya kazi yao. Ndio maana tunatoa wito wa kuachiliwa mara moja," afisa huyo amesem wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Jens Stoltenberg amesema anatarajia suala la kuzuiliwa kwa mwandishi wa gazeti la Wall Street Journal litajadiliwa wakati wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa NATO siku ya Jumanne, siku ambayo Finland itakuwa mwanachama wa 31 wa jumuiya hii.

Mkuu wa diplomasia ya Urusi na mwenzake wa Marekani, Sergei Lavrov na Antony Blinken, walizungumza juu suala la kuzuiliwa kwa mwandishi huyo wa habari siku ya Jumapili wakati wa mazungumzo ya nadra ya simu. Bw Lavrov alikariri mashtaka ya ujasusi yaliyotolewa dhidi ya mwandishi huyo wa habari na mamlaka ya Urusi, huku Bw Blinken akitaka tena kuachiliwa kwake mara moja, akilaani "kizuizi kisichokubalika".

Moscow pia ililaani "malalamiko ya vyombo vya habari" katika nchi za Magharibi yaliyosababishwa na kukamatwa kwa mwandishi huyu wa habari wa Marekani, tukio linalokuja katika hali ya kuongezeka kwa ukandamizaji nchini Urusi dhidi ya waandishi wa habari tangu kuanza kwa mashambulizi dhidi ya Ukraine mwzi Februari 2022.

Evan Gershkovich, mwandishi wa habari mwenye umri wa miaka 31 anayezungumza Kirusi, alitupilia mbali mashtaka dhidi yake wakatialiposikilizwa na mahakama ya Moscow siku ya Alhamisi, kulingana na shirika la habari la Urusi Tass. Mwandishi huyo wa habari wa Marekani amezuiliwa rumande katika gereza la Moscow hadi Mei 29, hatua ambayo inaweza kurefushwa kuzuiliwa kwake katika kusubiri kesi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.