Pata taarifa kuu

Urusi: Polisi wanamzuilia mwanamke mmoja baada ya tukio la shambulio

NAIROBI – Nchini Urusi, Polisi wamemzuia mwanamke mmoja baada ya tukio la shambulio lililomuua Vladlen Tatarsky, mwandishi wa mitandaoni anayeunga mkono vita nchini Ukraine.

Mwanablogu wa Urusi Vladlen Tatarsky ameuawa katika shambulio
Mwanablogu wa Urusi Vladlen Tatarsky ameuawa katika shambulio REUTERS - ANTON VAGANOV
Matangazo ya kibiashara

Mkanda wa video uliotolewa baada ya tukio hilo kutokea mkahawani mjini Saintt Petersburg, mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Darya Trepova, anasikika akikiri kuwa alitoa kilipuzi hicho.

Baadaye anasikika akisema kuwa, hafahamu iwapo kulikuwa na shambulio na hakiri tena kulitekeleza.

Mbali na kuawa kwa ya mwandishi huyo, watu wengine zaidi ya 30 walijeruhiwa katika tukio hilo.

Serikali ya Moscow, inasema kitendo hicho ni cha kigaidi na kuishtumu Ukraine kwa kuhusika na uchunguzi unaendelea kubaini mengi kuhusu shambulio hilo.

Aidha, Moscow imesema shambulio hilo limetekelezwa na vikosi maalum vya Ukraine kwa ushirikiano na kiongozi wa upinzani, Alexei Navalny.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.