Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Emmanuel Macron afanya ziara ya serikali nchini Uholanzi

Siku chache baada ya kurejea kutoka China, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anasafiri kenda nchini Uholanzi siku ya Jumanne kwa ziara ya kiserikali, ikiwa ni ziara ya kwanza ya rais wa Ufaransa katika ufalme wa Uholanzi kwa miaka ishirini na tatu.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kwenye ngazi za ikulu ya Élysée, Aprili 3, 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kwenye ngazi za ikulu ya Élysée, Aprili 3, 2023. AP - Aurelien Morissard
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameanza ziara ya kiserikali ya siku mbili nchini Uholanzi Jumanne (Aprili 11), ziara ya kwanza kwa rais wa Ufaransa nchini Uholanzi katika kipindi cha miaka ishirini na tatu. Zaiara hii itajikita zaidi masuala ya Ulaya na itakuwa fursa ya kufafanua matamshi yake yenye utata aliyotoa wakati wa ziara yake nchini China.

Rais, ambaye alirejea kutoka Beijing, na mkewe Brigitte, wamekaribishwa kwa heshima za kijeshi na nyimbo za kitaifa katika Ikulu ya Kifalme huko Amsterdam saa tano mchana na Mfalme Willem-Alexander na mkewe Maxima.

Mamia ya watu walikusanyika nyuma ya vizuizi chini ya jua kali lwakiwashangilia marais hao na wake zao, mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP amebainisha.

Baada ya tafrija iliyofuatwa na chakula cha mchana cha faragha, Mfalme wa Uholanzi na mkewe watatoa chakula cha jioni cha serikali kwa heshima yao Jumanne, pamoja na, kati ya wageni mashuhuri, mwaamuziki Dave, mwenye asili ya Uholanzi na maarufu sana nchini Ufaransa na mkurugenzi wa mashindano ya Basikeli ya Tour de France, Christian Prudhomme.

Emmanuel Macron atatoa hotuba alasiri juu ya uhuru wa kiuchumi na viwanda barani Ulaya, katika mlolongo wa ile ya La Sorbonne mnamo 2017.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.