Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Emmanuel Macron atoa wito kwa Xi Jinping 'kuishawishi Urusi'

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye yuko ziarani nchini China tangu siku ya Jumatano, amekutana na Xi Jinping Alhamisi hii, Aprili 6.  

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amezungumza na mwenzake wa China Xi Jinping kwa saa moja na dakika thelathini huko Beijing mnamo Aprili 6, 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amezungumza na mwenzake wa China Xi Jinping kwa saa moja na dakika thelathini huko Beijing mnamo Aprili 6, 2023. REUTERS - GONZALO FUENTES
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa ametangaza mjini Beijing kwamba ana imani na mwenzake wa China "kuishawishi Urusi kuachana na vita yake" dhidi ya Ukraine, zaidi ya mwaka mmoja baada ya kuanza kwa uvamizi Moscow nchini humo.

Kama ilivyotarajiwa, baada ya mahojiano ya kwanza Alhamisi na Waziri Mkuu wa China Li Qiang, Emmanuel Macron amekutana na Xi Jinping, aliyechaguliwa tena chini ya mwezi mmoja uliopita kwa muhula wa tatu kama Rais wa Jamhuri ya Watu wa China. Kama alivyongea na Li Qiang, rais wa Ufaransa amejadili vita vya Ukraine na rais wa China.

Kwa kuwa China bado ni mshirika muhimu wa Urusi na isiyeegemea upande wowote kuhusu vita vya Ukraine, Emmanuel Macron anatumai kuwa uhusiano huu na nafasi ya Xi Jinping ambaye alionyesha kumuunga mkono Rais wa Urusi Vladimir Putin wakati wa ziara yake mwezi Machi - huenda hili likaongoza kwa utulivu katika vita vya Ukraine, karibu miezi kumi na nne baada ya kuanza kwa uvamizi wa Urusi.

"Najua nina imani na wewe kuishawishi Urusi kua kwenye meza ya mazungumzo," rais wa Ufaransa amesema wakati wa mkutano huu wa nchi mbili huko Beijing. Kila mmoja ametoa wito wa mazungumzo ya amani.

"Kuanza tena kwa majadiliano haraka iwezekanavyo ili kujenga amani ya kudumu" ni muhimu, kwa maneno ya Emmanuel Macron. Xi Jinping ameomba "kuanzishwa upya kwa mazungumzo ya amani haraka iwezekanavyo".

Viongozi hao wawili wamefutilia mbali njia yoyote ya kutumia silaha za nyuklia, tishio ambalo tayari lilitolewa mara kadhaa na Kremlin. "Silaha za nyuklia haziwezi kutumika," amesema Xi Jinping, ambaye pia ameshutumu "mashambulizi yoyote kwa raia" na "matumizi yoyote ya silaha za kibiolojia na kemikali". Kwa upande wa Emmanuel Macron amesema, "ni wazi, nishati ya nyuklia lazima iondolewe kabisa kwenye mzozo huu".

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.