Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Ufaransa yakusudia kuendelea kuwa 'mshirika hai' wa Afrika

Ufaransa inakusudia kuendelea kuwa 'mshirika hai' wa Afrika, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Catherine Colonna amesema siku ya Jumatano, wakati Paris inakabiliwa na changamoto nyingi kwa sera yake kuhusu Afrika.

Emmanuel Macron na mwenzake wa Gabon Ali Bongo Ondimba katika ikulu ya rais huko Libreville mnamo Machi 1, 2023.
Emmanuel Macron na mwenzake wa Gabon Ali Bongo Ondimba katika ikulu ya rais huko Libreville mnamo Machi 1, 2023. © LUDOVIC MARIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Tuna washirika, changamoto za pamoja na mali za kutumia. Ni kwa kujumlisha vitendo vyetu vyote ndipo tutabaki kuwa washirika hai katika bara hili", ametangaza mkuu wa diplomasia ya Ufaransa mbele ya Bunge la Seneti, akijibu swali la seneta wa chama cha Les Republicains, Alain Joyandet.

Kauli yake inakuja wakati hisia dhidi ya Ufaransa ikienea katika nchi kadhaa barani Afrika, wakati uhusiano unadorora kwa wakati mmoja kwa nchi za Morocco na Algeria, wakati Ufaransa iko katika mchakato wa kufikiria upya uwepo wake wote wa kijeshi katika bara hilo, na kwamba nchi kama vile China, Urusi au Uturuki zikiendelea kupanua ushawishi wao.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wiki iliyopita alizuru Gabon, Angola, Kongo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kwa lengo la kujenga upya uhusiano na bara hili, ambalo Ufaransa ni mshirika muhimu wa kimataifa.

Katika miaka ya hivi karibuni, Ufaransa imejaribu kuachana na "Françafrique", mazoea yake yasiyoeleweka na mitandao yake ya ushawishi iliyorithiwa kutoka kwa ukoloni. Lakini katika bara hilo, baadhi ya sauti bado zinamkosoa Emmanuel Macron kwa kuendeleza mikutano yake na viongozi wa Afrika wanaochukuliwa kuwa wa kiimla.

"Ufaransa imebadilika, tunataka kuondoka kwenye maono haya ya zamani", amesema Catherine Colonna. Paris pia inadai kwamba baadhi ya washirika, kama vile kundi la wanamgambo wa Urusi Wagner, wanachochea hisia za chuki dhidi ya Ufaransa katika baadhi ya nchi za Kiafrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.