Pata taarifa kuu

Macron ahaidi msaada wa fedha kumaliza mzozo wa mashariki ya DRC

NAIROBI – Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anayezuru jijini Kinshasa, ameahidi kuwa nchi yake itatoa Euro Milioni 34 kusaidia kutafuta amani Mashariki mwa DRC, huku akisisitiza kuwa wanaoendelea kurudisha nyuma jitihada za kupata amani wanapaswa kuwekewa vikwazo. 

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa DRC  Félix Tshisekedi, Tarehe 4 Machi jijini Kinshasa.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa DRC Félix Tshisekedi, Tarehe 4 Machi jijini Kinshasa. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Macron ametoa ahadi na kauli hiyo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Felix Thisekedi, wakati huu kukiwa na dhana kuwa Ufaransa inaiunga mkono Rwanda, inayodaiwa kuwaunga mkono waasi wa M 23. 

Alipoulizwa kutamka wazi, kuhusu Rwanda kuwaunga mkono waasi hao, madai ambayo Kigali inakanusha, amesema nchi yake tayari imeweka wazi msimamo wake kuhusu kundi hili na wale wanaoliunga mkono. 

“Ningependa leo Ufaransa ibaki mwaminifu katika ushirikiano wake wake wa Kuisaidia DRC kulinda uadilifu na mamlaka yake. Kuporwa kwa DRC kunapaswa vifika mwisho. Hakuna swala la kufikiria kugawa nchi au vita.” amesema rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

00:21

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Kuhusu DRC

Naye rais Thisekedi, amewashatumu waasi hao kuendelea kwenda kinyume na mikata ya Nairobi na Luanda, kuweka silaha chini na kuondoka katika maeneo wanayoshibiti. 

“Kuhusu swala la huu uchokozi usio wa haki, mimi nasalia na msimamo wangu kwa sababu kama Kusitisha vita tulikuwa tayari tumeshachukuwa uamuzi tangu mazungumzo ya Nairobi, kisha ya Luanda, kutaka waasi wa ondoke, lakini hakuna ambacho kimefanyika, tuipe amani fursa. “amesema rais Thisekedi

00:24

Rais wa DRC Felix Thisekedi Kuhusu M23

Macron anarejea jijini Paris baada ya kumaliza ziara yake katika mataifa ya Afrika ya Kati, DRC ikiwa nchi yake ya mwisho, akiwa na ujumbe kuwa, muda wa mataifa ya Afrika kulazilimishwa cha kufanya, umepitiwa na wakati. 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.