Pata taarifa kuu

Ziara ya rais Macron: Mashirika ya kiraia DRC yaomba msaada kutoka Ufaransa

NAIROBI – Mashirika ya kiraia zaidi ya 150 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, yametia saini azimio la kumtaka rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, kulaani nchi ya Rwanda kutokana na madai ya mchango wake katika mapigano yanayoendelea Mashariki mwa DRC.

Rais Emmanuel Macron katika Ikulu ya Elysee 27/04/2021
Rais Emmanuel Macron katika Ikulu ya Elysee 27/04/2021 AP - Thibault Camus
Matangazo ya kibiashara

Mashirika hayo pia yamemtaka Macron, ambaye anatarajiwa jijini Kinshasa Jumamosi, kuunga mkono taifa hilo liwekewe vikwazo kutokana na madai ya kuwasaidia waasi wa M23.

Kadhalika, yameiomba Ufaransa, kulisaidia jeshi la nchi hiyo katika vita dhidi ya makundi yenye silaha mashariki mwa nchi hiyo, kama anavyosema hapa wakili George Kapiamba, mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu na mwenyekiti wa shirika la ACAJ lenye makao jijini Kinshasa.

Tumetoa taarifa hii kjwa vyombo vya habari kama kama sehemu ya mtandao wetu dhidi ya ugaidi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa ziara ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron huko Kinshasa, kumwomba alaani uchokozi wa Rwanda, kuunga mkono wito wa vikwazo katika ngazi ya Umoja wa Mataifa dhidi ya Rwanda na viongozi wake. Amesema Kapiamba.

Kapiamba anasema kulingana naye, mashirika hayo yanaamini kwamba iwapo rais Macron hatafanikiwa kufanya yale wanayolalamikia, basi wataichukulia ziara yake kama isiyo ya manufaa makubwa kwa raia wa Kongo, na wataiomba serikali kuangazia upya ushirikiano na Ufaransa.

Wito wa wanaharakati hawa umeonekana kuungwa mkono na aliyekuwa rais wa Ufaransa François Hollande, ambapo akizungumza kwenye kituo cha habari cha ufaransa Alhamisi wiki hii, alisema anatumai Macron atatoa hotuba kuhusu mapigano haya mashariki mwa DRC ambayo yamewaathiri watoto na wanawake.

Kulingana na ratiba ya ziara ya Macron katika mataifa manne barani Afrika, siku ya Jumamosi atakuwa anakamilisha ziara yake nchini DRC baada ya kuzuru, Gabon, Angola na jamhuri ya Kongo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.