Pata taarifa kuu

ICC yafutilia mbali 'vitisho' kufuatia hati ya kukamatwa kwa Vladimir Putin

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetupilia mbali siku ya Jumatano hii, Machi 22, 2023 'vitisho' na hatua zilizotangazwa dhidi ya mwendesha mashtaka wake na majaji waliohusika katika utoaji wa hati ya kukamatwa kwa Vladimir Putin kwa uhalifu wa kivita wakati wa uvamizi wa Urusi.

Mwendesha Mashtaka wa ICC Karim Khan mnamo Septemba 26, 2022 huko Hague, Uholanzi.
Mwendesha Mashtaka wa ICC Karim Khan mnamo Septemba 26, 2022 huko Hague, Uholanzi. © Peter Dejong/AP
Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya Baraza la mataifa wanachama wa Mahakama hiyo, ambayo ni taasisi yake ya kutunga sheria, "inachukizwa na majaribio haya ya kuzuia juhudi za kimataifa za kupata uwajibikaji kwa vitendo vinavyokatazwa na sheria ya kimataifa ya jumla", ofisi hyo imesema.

Chombo cha kutunga sheria cha Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu siku ya Jumatano kimeshutumu "vitisho" kutoka Urusi dhidi ya wanachama wa ICC baada ya kutoa hati ya kukamatwa kwa Vladimir Putin kwa uhalifu wa kivita kwa "kuwateka nyara" watoto wa Ukraine.

Urusi ilitangaza Jumatatu kufunguliwa kwa uchunguzi wa jinai dhidi ya mwendesha mashtaka na majaji watatu wa mahakama ya ICC, baada ya mahakama hii kutoa hati ya kukamatwa kwa rais wa Urusi na kamishna wake wa haki za mtoto, Maria Lvova-Belova. Rais wa zamani wa Urusi Dimitri Medvedev, nambari 2 wa sasa wa Baraza la Usalama la Urusi, ambaye amezoea kutoa taarifa za kushangaza, kulingana na vyombo vya habari vya Uholanzi siku hiyo aliwashauri majaji wa ICC kwenye Telegram "kuangalia kwa makini angani", akimaanisha uwezo wa mashambuliaji ya Urusi. Chombo cha kutunga sheria cha ICC katika taarifa kimesema kinsikitishwa na "majaribio ya kuzuia juhudi za kimataifa kuhakikisha uwajibikaji kwa vitendo vinavyokatazwa na sheria ya kimataifa". Bunge pia "limethibitisha tena imani yake kamili kwa mahakama".

Mwendesha mashitaka wa ICC, Karim Khan, ambaye amekuwa akichunguza uwezekano wa uhalifu wa kivita au uhalifu dhidi ya binadamu uliofanywa wakati wa mashambulizi ya Urusi nchini Ukaine kwa zaidi ya mwaka mmoja, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba idadi ya madai ya kupelekwa kwa watoto wa Ukraine hadi Urusi au maeneo inakodhibiti "ilifikia maelfu" . Kulingana na Kiev, zaidi ya watoto 16,000 wa Ukraine wamepelekwa nchini Urusi tangu uvamizi wa Februari 24, 2022, ambao wengi wao wamewekwa katika vituo vya kulea watoto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.