Pata taarifa kuu
URUSI- UKRAINE MAPIGANO

Ukraine: Idadi ya waliofariki katika shambulio la urusi imefikia watu 8

Ofisi ya rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky inasema kuwa watu 8 wameuawa katika shambulio la roketi lilotekelezwa na wanajeshi wa Urusi katika eneo la Vinnytsia.

Eneo la Chasiv Yar, mjini  Donetsk nchini Ukraine baada ya shambulio la roketi za Urusi Julai 10, 2022
Eneo la Chasiv Yar, mjini Donetsk nchini Ukraine baada ya shambulio la roketi za Urusi Julai 10, 2022 REUTERS - GLEB GARANICH
Matangazo ya kibiashara

Polisi inasema makazi ya raia yameharibiwa katika shambulio hilo la roketi tatu zililolenga jengo moja katika eneo hilo.

Watoa huduma za dharura wanaeleza kuwa raia 8 walifariki wakati wa tukio hilo wengine 8 wakiripotiwa kujeruhiwa.

Shambulio hili linakuja wakati huu ambapo maofisa wa serikali kutoka katika mataifa kadhaa wakikutana nchini Uholanzi kwa ajili ya mazungumzo na mkuu wa mahakama ya kimataifa kuhusu jinai ICC kujadili namna ya kuwafungulia mashataka wahusika wa uhalifu wa kibindamu nchini Ukraine.

Tangu rais Vladimir Putin kuwatuma wanajeshi wake nchini Ukraine Feburuari 24, wanajeshi wake wametuhumiwa kwa kuhusika na visa vya ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo.

Vikosi vya urusi vikituhumiwa pia kwa kuhusika katika mauwaji ya raia wasio na hatia jijini Kyiv likiwemo shambulio la bomu katika ukumbi wa sinema Machi 16 mjini Mariupol.

Mataifa 40 kutoka katika muungano wa EU na sehemu zengine za ulimwengu wanashiriki katika kikao hicho chini ya uwenyeji wa waziri wa mambo ya kigeni wa Uholanzi Wopke Hoekstra, mwendesha mashtaka wa ICC Karim Khan na kamishena wa EU kuhusu masuala ya haki EU Didier Reynders.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.