Pata taarifa kuu

Ukraine: ICC yatoa hati ya kukamatwa dhidi ya Putin

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) imesema siku ya Ijumaa Machi 17 kwamba imetoa hati ya kukamatwa dhidi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa jukumu lake katika uhalifu wa kivita uliofanywa nchini Ukraine tangu uvamizi wa Urusi.

Ras wa Urusi Vladimir Putin alengwa na hati ya kukamatwa ya ICC.
Ras wa Urusi Vladimir Putin alengwa na hati ya kukamatwa ya ICC. AFP - MIKHAIL KIREYEV
Matangazo ya kibiashara

"Leo, Machi 17, 2023, Chumba cha II cha Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita kimetoa maagizo ya kukamatwa dhidi ya watu wawili kama sehemu ya hali nchini Ukraine: Bwana Vladimir Vladimirovitch Putin na Bi Maria Alekseyevna Lvova-Belova" Kamishna kiongozi wa Haki za mtoto nchini Urusi, imesema ICC katika taarifa.

Bwana Putin "anadhaniwa kuwajibika kwa uhalifu wa vita kwa kuwadhibiti kinyume cha sheria raia (watoto) na uhamishaji haramu wa raia (watoto) wa maeneo yaliyochukuliwa ya Ukraine kwa Shirikisho la Urusi," imeongeza ICC.

"Uhalifu huo ultekelezwa kwenye maeneo ya Ukraine yaliyochukua angalau kuanzia Februari 24, 2022", imebainisha ICC, na kuongeza kuwa kunana "sababu nzuri za kuamini kwamba Bwana Putin anawajibika kwa uhalifu uliotajwa hapo awali".

Gazeti la New York Times liliripoti siku ya Jumatatu kwamba ICC inajiandaa kuzindua mashtaka dhidi ya Warusi kwa kuhamisha watoto kwenda Urusi na kwa mashambulizi ya angani kwa makusudi dhidi ya miundombinu ya kiraia huko Ukraine.

Mwendesha mashtaka wa CPI, Karim Khan alisema mapema mwezi huu baada ya ziara yake nchini Ukraine kwamba madai ya utekaji nyara wa watoto yalikuwa "mada ya uchunguzi wa kipaumbele". ICC, iliyoundwa mnamo 2002 kuhukumu uhalifu mbaya zaidi uliofanywa ulimwenguni, imekuwa ikichunguza kwa zaidi ya mwaka mmoja juu ya uhalifu wa kivita au dhidi ya uhalifu wa binadamu uliofanywa wakati wa mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine.

Urusi wala Ukraine sio wanachama wa ICC, lakini Kyiv ilikubali mamlaka ya mahakama hii kwenye ardhi yake na inafanya kazi na mwendesha mashtaka. Urusi inakanusha madai ya uhalifu wa kivita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.