Pata taarifa kuu

Uholanzi yafunga sehemu ya kibiashara ya ubalozi wa Urusi na kuwafukuza wanadiplomasia

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi imetangaza Jumamosi Februari 18 kufungwa kwa sehemu ya kibiashara ya ubalozi wa Urusi huko Amsterdam, pamoja na kufukuzwa kwa wanadiplomasia wa Urusi. Uholanzi inaishutumu Moscow kwa kuendelea kujaribu kutuma wapelelezi nchini humo.

Uholanzi inaishutumu Moscow kwa kuendelea kujaribu kutuma wapelelezi nchini humo.
Uholanzi inaishutumu Moscow kwa kuendelea kujaribu kutuma wapelelezi nchini humo. © M. Minderhoud
Matangazo ya kibiashara

Urusi pia inakataa kutoa visa ambavyo vitawaruhusu wanadiplomasia wa Uholanzi kufanya kazi huko Moscow, chanzo hicho kimeongeza, na kuongeza kuwa ubalozi mdogo wa Uholanzi huko Saint Petersburg utafunga kwa kukosa wafanyakazi.

Mwaka jana, baada ya uvamizi wa Moscow nchini Ukraine, nchi kadhaa za Ulaya zilitangaza kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi wanaoshukiwa kufanya ujasusi.

Ubelgiji, Uholanzi, Jamhuri ya Czech na Ireland zilitangaza kuwafukuza wanadiplomasia kadhaa wa Kirusi, katika hatua iliyoratibiwa.

Nchi nyingine, kama vile Marekani, Poland na nchi za Baltic ndio zilianza kutangaza kuwafukuza maafisa wa ujasusi wa Urusi tangu uvamizi wa Moscow nchini Ukraine ulioagizwa na Vladimir Putin mnamo Februari 24.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.