Pata taarifa kuu

Norway kutoa euro milioni 200 kusaidia Ukraine kujipatia gesi

Norway itatoa euro milioni 205 kusaidia Ukraine kujipatia gesi wakati msimu wa baridi unapokaribia, ametangaza Waziri Mkuu wa Norway, Jonas Gahr Støre, katika taarifa kwa vyombo vya habari.

aziri Mkuu wa Norway, Jonas Gahr Støre.
aziri Mkuu wa Norway, Jonas Gahr Støre. AP - Marit Hommedal
Matangazo ya kibiashara

"Vita hivyo vimeifanya Ukraine kuhitaji msaada kutoka nje. Ukraine imeiomba Norway kuchukua nafasi ya uongozi katika kupata upatikanaji wa nishati. Tunaitikia na tunajitolea kutoa euro bilioni 200 ili wananchi wa Ukraine waweze kununua gesi msimu huu wa kiangazi na msimu wa baridi."

Bahasha hii, iliyochukuliwa kutoka kwa msaada wa jumla wa bilioni 10 pesa za Norway zilizoahidiwa na Norway kwa Ukraine, zitalipwa kwa Benki ya Ulaya ya Ujenzi na Maendeleo (EBRD), ambayo itakuwa na jukumu la ununuzi wa gesi.

"Mchango wetu katika ununuzi wa gesi utasaidia hasa kupasha joto hospitali na shule nchini Ukraine msimu huu wa baridi na kuhakikisha uwezekano wa kutengeneza vyakula vya moto," Støre amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.