Pata taarifa kuu

Ukraine: Hatari ya 'dutu zenye mionzi' kwenye kinu cha nyuklia cha Zaporizhia

Kuna hatari ya "kunyunyizia dutu zenye mionzi" kwenye kinu cha nyuklia cha Ukraine huko Zaporizhia, kinachokaliwa na wanajeshi wa Urusi, kampuni ya nyuklia ya serikali ya Ukraine Energoatom, imesema Jumamosi hii Agosti 27.

Askari wa Urusi akiwa katika doria karibu na kinu cha nyuklia cha Zaporizhia mnamo Mei 1, 2022.
Askari wa Urusi akiwa katika doria karibu na kinu cha nyuklia cha Zaporizhia mnamo Mei 1, 2022. © Andrey Borodulin, AFP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Energoatom, wanajeshi wa Urusi "wameshambulia mara kadhaa kwa siku ya mwisho" eneo hili. "Miundombinu ya ya kinu hiki imeharibiwa, na kuna hatari za kuvuja kwa hidrojeni na kunyunyizia vitu vyenye mionzi," Energoatom imesema kwenye Telegram, na kuongeza kuwa kulikuwa na "hatari kubwa ya tukio la moto mkubwa". Na, tangu Jumamosi alasiri (saa 9 alasiri UT), kinu cha nyuklia cha Ukraine huko Zaporizhia "hufanya kazi kwa hatari ya kukiuka viwango vya usalama katika suala la mionzi na moto", imeripoti kampuni ya Energoatom.

Makombora kumi na saba

Urusi kwa upande wake pia imeishutumu Ukraine kwa kushambulia kwa makombora Zaporizhia katika muda wa saa 24 zilizopita. Katika taarifa yake, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imehakikisha kwamba jeshi la Ukraine lilifyatua makombora kumi na saba kwenye uzio wa mtambo huo mkubwa zaidi barani Ulaya. "Makombora manne yalianguka juu ya paa la jengo maalum namba moja ambapo kunapatikana kiwanda cha kuyeyusha nyuklia ya Marekani cha kampuni ya  Westinghouse, Urusi imebaini na kuongeza kwamba makombora yaliyosalia yalianguka na kulipuka mita thelathini na ghala la mafuta ya kutumia karibu na lingine lililokuwa na "mafuta safi".

Kulingana na jeshi la Urusi, jeshi la Ukraine limefyatua risasi kutoka karibu na mji wa Marhanet, ambao unasogelea kinu hiki, kwenye ukingo wa pili wa mto wa Dnieper ambao bado unadhibitiwa na Kyiv. Shirika la habari la AFP halikuweza kuthibitisha taarifa hizi kutoka chanzo huru. Kiwanda cha Zaporizhia, ambapo mitambo sita kati ya kumi na tano ya Ukraine ipo, kilichukuliwa na wanajeshi wa Urusi mapema mwezi wa Machi, muda mfupi baada ya uzinduzi wa uvamizi mnamo Februari 24, na kiko karibu na uwanja wa vita kusini mwa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.