Pata taarifa kuu

Vladimir Putin atia saini agizo la kuongeza idadi ya wanajeshi wa Urusi

Vladimir Putin alitia saini siku ya Alhamisi agizo la kuongeza idadi ya wanajeshi katika jeshi la Urusi kwa 10% mnamo Januari 1, 2023. Tangazo kali ambalo linakuja katikati ya mzozo wa Ukraine, na wakati kwenye uwanja wa vita kuna maendeleo katika wiki za hivi karibuni.

Gwaride la askari wa Urusi katika kuunga mkono askari wanaopambana nchini Ukraine, huko Volgograd, Julai 11, 2022.
Gwaride la askari wa Urusi katika kuunga mkono askari wanaopambana nchini Ukraine, huko Volgograd, Julai 11, 2022. AP - Alexandr Kulikov
Matangazo ya kibiashara

Jeshi litalazimika kuwa na wanajeshi milioni mbili, wakiwemo wanajeshi milioni 1.15, dhidi ya milioni 1.9, wakiwemo wapiganaji zaidi ya milioni moja, mwaka 2017, kulingana na agizo hili lililochapishwa na serikali na kuanza kutumika Januari 1, 2023, bila kuhesabu wafanyakazi wa kiraia, hili ni ongezeko la askari 137,000, au zaidi ya sehemu ya kumi ya jeshi la sasa. Haijulikani ni wanajeshi wangapi watapelekwa nchini Ukraine, wala kama Vladimir Putin atakusudia kutumia jeshi hilo kuimarisha wanajeshi wake.

"Vikosi vya Urusi ambavyo vimehusika tangu Februari 24 katika operesheni maalum ya kijeshi dhidi ya Ukraine vimepata hasara kubwa sana, na Moscow inapata shida kuajiri wanajeshi wapya," anabainisha Jenerali Jérôme Pellistrandi, mhariri mkuu wa Gazeti la "Defense Nationale" (Ulinzi wa taifa). Vladimir Putin pia anatambua kwamba ameingia katika makabiliano si ya moja kwa moja na NATO, bali makabiliano yasiyo ya moja kwa moja, na kwamba vikosi vyake vinavyohusika katika vita ambavyo ni karibu sawa na idadi ya wanajeshi wa Ukraine, hawana uwezo wa kutosha kuhakikisha usalama wa Urusi. "

Mapigano yarindima kusini na mashariki mwa Ukraine

Sababu za hatua hii hazijaelezwa katika agizo. Kwa muda wa miezi sita, mashambulizi nchini Ukraine kwa kweli yamekuwa ya gharama kubwa sana katika suala la rasilimali watu na vifaa. Baada ya kushindwa kudhibiti mji wa Kyiv mwanzoni mwa uvamizi huo, vikosi vya Moscow sasa vinaelekeza nguvu zao mashariki na kusini mwa Ukraine, ambapo wamesonga mbele kidogo katika wiki za hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.