Pata taarifa kuu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ashutumu 'vita vya kipuuzi' nchini Ukraine

Wakati mzozo wa Ukraine ukiingia mwezi wa saba, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kuwepo kwa amani mbele ya Baraza la Usalama. Antonio Guterres anasema ana wasiwasi hasa kuhusu hatari ya nyuklia katika kinu cha nguvu cha Zaporijgia.

Antonio Guterres wakati wa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mnamo Agosti 24.
Antonio Guterres wakati wa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mnamo Agosti 24. Getty Images via AFP - MICHAEL M. SANTIAGO
Matangazo ya kibiashara

Kwa mara nyingine tena, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili wasiwasi kuhusu vita vya Ukraine, anaripoti mwandishi wetu wa habari huko New York, Loubna Anaki. Kwa mara nyingine tena, mijadala ilimalizka bila jibu. Mkutano huu ulioambatana na Siku ya Uhuru wa Ukraine, ulifanyika Jumatano hii, Agosti 24, mbele ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Akiwa amerudi kutoka Ukraine, Antonio Guterres aliwasilisha ripoti yake kuhusu hali hiyo kwa wajumbe wa Baraza. "Leo ni hali ya kusikitisha na yenye huzuni, miezi sita tangu Urusi ilipovamia Ukraine mnamo Februari 24," alisema, akishutumu "athari za vita hivi visivyo na maana, mbali zaidi ya Ukraine".

Hasa, alirejelea "wasiwasi wake mkubwa" juu ya shughuli za kijeshi karibu na kituo cha nyuklia cha Zaporijgia. "Kuongezeka zaidi kwa hali hiyo kunaweza kusababisha vifo vingi," alisema.

"Vita isiyo na msingi na ya kikatili"

Antonio Guterres pia alitoa sasisho juu ya kuanza tena mauzo ya nafaka kutoka bandari ya Odessa na kusisitiza juu ya hatari ya kuongezeka kwa shida ya chakula. "Ikiwa hali hii itaendelea, hakutakuwa na chakula cha kutosha mwaka 2023," mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alisema.

Mgogoro wa chakula ambao rais wa Ukraine pia alirejelea, ambaye alihutubia Baraza kwa njia ya video. "Ulimwengu unaona jinsi unategemea uhuru wetu," Volodymyr Zelensky alisema. Kwa upande wao wanachama wengine wa Baraza la Usalama wametoa wito wa kusitishwa kwa vita hivyo. "Vita visivyo na msingi na vya kikatili", kulingana na mwakilishi wa Marekani.

Akishutumu "kampeni" ya nchi za Magharibi "kuidharau" Urusi, Vassily Nebenzia, balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, alilaumu jukumu lote la vita vya Ukraine. Katika taarifa ya pamoja iliyosomwa na balozi wa Ukraine baada ya mkutano huo, baadhi ya nchi hamsini zikiwemo za Ulaya, Japan, Marekani, Colombia, Uturuki au Korea Kusini "zilirejelea matakwa yao ya Urusi kusitisha mapigano mara moja dhidi ya Ukraine".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.