Pata taarifa kuu

EU yaonyesha uungaji wake mkono kwa Ukraine na hatua kali dhidi ya Urusi

Vita nchini Ukraine vimekuwa vikiendelea kwa miezi sita sasa na Umoja wa Ulaya uko mstari wa mbele. Umoja huo umethibitisha kuunga mkono Ukraine na kuchukua vikwazo ambavyo havijawahi kushuhudiwa dhidi ya Urusi.

Wabunge wa Ulaya wakimpigia makofi Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakati wa hotuba yake ya mkutano wa video mbele ya Bunge la Ulaya Machi 1.
Wabunge wa Ulaya wakimpigia makofi Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakati wa hotuba yake ya mkutano wa video mbele ya Bunge la Ulaya Machi 1. AFP - JOHN THYS
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Baraza hilo Charles Michel alithibitisha Jumanne Agosti 23, wakati wa kongamano la Crimea lililoandaliwa na Volodymyr Zelensky, kwamba Umoja wa Ulaya (EU) ulisema kwa sauti kubwa na wazi tangu siku za kwanza za mzozo huo kwamba Ukraine ni mali ya "familia ya Umoja wa Ulaya. ". Tamko hili sio tu kwamba lina thamani ya kisiasa, pia linaakisi jiografia ya bara na wakati huu nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wamechukua majukumu yao.

Kuhusika huku kwa EU kunakuja miaka thelathini baada ya kuanza kwa vita vya Yugoslavia, vita katikati mwa bara na ambapo Ulaya wakati huo ilikuwa imekumbwa kwa zaidi ya miaka mitatu kwa ukimya na udhaifu wake. Tofauti ni ya kushangaza tangu, kwa mfano, Umoja wa Ulaya ulitangaza vikwazo vya kwanza tangu mwanzo na vitendo vimeendelea kufuata kwa miezi sita.

Vikwazo "vikubwa" dhidi ya Urusi

Vikwazo hivi, Umoja wa Ulaya ulitangaza tangu siku ya kwanza kwamba vitakuwa "vikubwa" na havitaacha kuimarishwa. Vikwazo vya kwanza vya Ulaya vilianza kutekelezwa siku moja kabla ya kuingia kwa askari wa Urusi nchini Ukraine. Vikwazo hivi viliamuliwa kutokana na kutambuliwa na Urusi kwa jamhuri za kujitenga za Luhansk na Donetsk.

Vita nchini Ukraine

Tangu wakati huo, EU imeendelea kuimarisha vikwazo hivyo na mwishoni mwa mwezi wa Julai, ulikuwa kwenye seti ya saba ya vikwazo hivyo. Kwanza kabisa, kuna vikwazo vya kibinafsi ambavyo sasa vinaathiri Warusi 1,214 waliopigwa marufuku kuishi Ulaya na ambao mali zao katika Umoja wa Ulaya zimezuiwa, kati yao viongozi wengi wa kisiasa na kijeshi na washirika wa karibu wa Kremlin. Kuna vikwazo vya kibiashara hasa, pamoja na kupigwa marufuku kwa anga ya Ulaya kwa ndege za Urusi na kupiga marufuku meli za Urusi kutia naga kwenye bandari za wanachama wa Umoja wa Ulaya. Na pia kwa kupiga marufuku matangazo ya vyombo vya habari vya propaganda vya Kirusi Sputnik na Russia Today.

Gharama kubwa ya kiuchumi

Lakini msimamo huu wa vikwazo bado unakuja na gharama kubwa ya kiuchumi kwa Umoja wa Ulaya. Miongoni mwa vikwazo, kuna vikwazo vya mafuta na makaa ya mawe ya Urusi, na vikwazo hivi vilifuatiwa na ulipizaji kisasi kwa kukatwa hatu kwa hatua kwa bomba la gesi kwa nchi kumi na mbili wanachama wa Umoja wa Ulaya, kwanza Bulgaria na Poland hadi Ufaransa, Uholanzi au Finland, kwa mfano.

Mkuu wa diplomasia ya Ulaya Josep Borrell alisema mnamo Agosti 23 kwamba Ulaya tayari imeweza kufanikiwa bila 50% ya uagizaji wa gesi ya Urusi, lakini muswada huo ni mzito kwa wanaviwanda wa Ulaya. Hali hii pia imesababisha Umoja wa Ulaya kuchukua maamuzi ambayo hayajawahi kushuhudiwa kujenga hifadhi ya gesi na kuzindua upya vituo vya nishati ya makaa ya mawe, lakini pia nishati ya nyuklia.

Licha ya hayo, Umoja wa Ulaya uliweza kuhifadhi umoja wake wa kisiasa hata kama kulikuwa na mvutano, hasa juu ya athari za kiuchumi za vikwazo, na mijadala mirefu mwezi Juni na Hungary. Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wanaonyesha msimamo mmoja dhidi ya Moscow na uimara huu wa kidiplomasia hauna mfano halisi. Jambo ambalo pia halijawahi kushuhudiwa ni kuzinduliwa upya kwa ulinzi wa Ulaya, ambao unaenda hata katika utoaji wa silaha na miradi ya mafunzo kwa jeshi la Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.