Pata taarifa kuu

Urusi: mamia ya watu washiriki mazishi ya Daria Dugina

Mazishi ya Daria Dugina, binti wa mwanafalsafa Alexander Dougin anayeunga mkono mashambulizi nchini Ukraine, yamefanyika Jumanne hii asubuhi Agosti 23 huko Moscow. Mamia kadhaa ya watu walikusanyika kutoa heshima zao za mwisho kwa mmwanake huyo mwenye umri wa miaka 29 aliyeuawa Jumamosi jioni katika mlipuko wa gari lake, shambulio ambalo Moscow inanyooshea kidole cha lawama Kyiv

Mwanafalsafa Alexander Dugin, kushoto, akihudhuria sherehe ya mwisho ya kumuaga binti yake Daria Dugina huko Moscow, Urusi, Jumanne, Agosti 23, 2022.
Mwanafalsafa Alexander Dugin, kushoto, akihudhuria sherehe ya mwisho ya kumuaga binti yake Daria Dugina huko Moscow, Urusi, Jumanne, Agosti 23, 2022. AP - Dmitry Serebryakov
Matangazo ya kibiashara

Wote waliohudhuria mazishi haya walivaa fulana nyeusi kwa sherehe hii chini ya ulinzi wa hali ya juu.

"Hakuhisi woga," baba yake amesema wakati wa kutoa heshima ya mwisho kwa binti yake. Mara ya mwisho tulipozungumza ilikuwa Jumamosi iliyopita, aliniambia: "Baba, najisikia kama shujaa, kama shujaa. Hivyo ndivyo ninavyotaka kuwa, sitaki hatima nyingine. Nataka kuwa na watu wangu, na nchi yangu". "

►Soma pia: Urusi yaishutumu Ukraine kwa kumuua binti wa mwanafalsafa Alexander Dugin

Taji la Ujasiri

Katika umati wa watu waliofika kutoa heshima zao za mwisho kwa Daria Dugina na kufanya gwaride mbele ya jeneza, walikuwepo ndugu wa familia lakini pia viongozi wa kisiasa. Rais Putin pia alimkabidhi baada ya kifo chake Jumatatu jioni taji la Ujasiri, taji muhimu nchini Urusi. Medali iliwekwa kwenye jeneza lake.

"Ulikuwa uhalifu wa kinyama ambao hauwezi kusamehewa (...). Hakuwezi kuwa na huruma kwa waandaaji, wafadhili na watekelezaji wa mauaji haya," Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.