Pata taarifa kuu

Urusi: Binti wa mshirika wa karibu wa Putin auawa katika mlipuko wa gari lake

Daria Dugina, binti ya Alexander Dougin, mshirika wa karibu wa Rais wa Urusi wa Urusi Vladimir Putin, aliuawa Jumamosi jioni Agosti 20 katika mlipuko wa gari alilokuwa akiendesha karibu na mji wa Moscow. 

Wachunguzi wanachunguza eneo ambapo mlipuko wa gari uliomuua Daria Duguina, binti wa mwanafalsafa Alexander Dugin, karibu na Moscow mnamo Agosti 21, 2022.
Wachunguzi wanachunguza eneo ambapo mlipuko wa gari uliomuua Daria Duguina, binti wa mwanafalsafa Alexander Dugin, karibu na Moscow mnamo Agosti 21, 2022. © Investigative Committee of Russia / via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Inadhaniwa babake, mwanafalsafa wa Kirusi Alexander Dugin ambaye anajulikana kama "Ubongo wa Putin," huenda ndiye aliyelengwa na shambulio hilo.

Bw Dugin ni mwana itikadi mashuhuri wa uzalendo na anaaminika kuwa karibu na rais wa Urusi.

Alikuwa ametetea kuvamiwa kwa Ukraine na anasifika kuwa na ushawishi mkubwa katika duru za siasa za kijiografia huko Moscow. Kulingana na wachunguzi wa Urusi, mlipuko huo ulitokana na bomu.

Karibu saa tatu usiku, mlipuko ulitokea kwenye barabara kuu ya mkoa wa Moscow. Kwenye gurudumu la gari, ambalo lilishika moto mara moja, alikuwa mwandishi wa habari mchanga na mwanasayansi wa kisiasa Daria Duguina, 30, ambaye si mwingine ila binti wa mwanafalsafa wa kitaifa wa Urusi na mwananadharia Alexander Dugin.

Kulingana na habari kutoka kwa vyanzo mbalimbali vya Telegraph vinavyojulikana kuwa karibu na serikali na baadaye kuthibitishwa na kituo cha Pervy Kanal, baba na binti walikuwa wakirudi kutoka kwa tamasha la "Mila", mkusanyiko wa utaifa wa Urusi katika viunga vya nje vya Moscow.

Alexander Dugin na binti yake walikuwa wakihudhuria tamasha katika shamba moja karibu na Moscow, ambapo mwanafalsafa huyo alitoa hotuba.

Tamasha la "Utamaduni" linajielezea tukio hilo kama la familia kwa wapenzi wa sanaa na hufanyika katika shamba la Zakharovo ambapo mshairi wa Kirusi Alexander Pushkin aliwahi kuishi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.