Pata taarifa kuu

Urudi yaonywa kutothubutu kushambulia kituo cha nyuklia cha Zaporizhzhia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress, ameitaka Urusi kutokata kituo cha nyuklia cha Zaporizhzhia kwenye njia kuu ya kusafirisha umeme nchini Ukraine.

Kituo cha nyuklia cha Zaporizhia, kinapatikana karibu na jiji la Enerhodar, mnamo Agosti 4, 2022.
Kituo cha nyuklia cha Zaporizhia, kinapatikana karibu na jiji la Enerhodar, mnamo Agosti 4, 2022. © Alexander Ermochenko/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Wito huu wa Guteress umekuja baada ya kutembelea bandari ya Odessa Kuisni mwa Ukraine, baada ya Urusi kuonya kuwa inapanga kukata njia kuu ya kusafirisha umeme kwenda Ukraine kwenye kituo hicho cha nyuklia. 

Aidha, Guteress amesema bado kuna kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha kuwa, dunia inapata nafaka kutoka Ukraine lakini pia chakula na mbolea kutoka nchini Urusi, hata baada ya mkataba ulioruhusu usafirishaji kuanza tena. 

Siku ya Alhamisi, Guteress akiwa na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan walikutana na kufanya mazungumzo na rais Volodymyr Zelenskyy kuhusu uwezekano wa kusitisha vita vinavyoendelea na kuongeza kiwango cha usafirishaji wa vyakula kwenda sehemu mbalimbali za dunia hasa barani Afrika, ili kukabiliana na ukame uliosababisha uhaba wa chakula. 

Wakati hayo yakijiri, jimbo la Crimea ambalo lilichukuliwa na Urusi mwaka 2014 limeendelea kushambuliwa huku milipuko ikisikika nje ya uwanja wa ndege wa kijeshi wa Belbek, ambao jeshi la Urusi hutumia kurusha makombora nchini Ukraine. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.