Pata taarifa kuu

Ukraine: Timu ya IAEA njiani kuelekea kituo cha nyuklia cha Zaporizhia

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) ametangaza leo Jumatatu asubuhi kwamba ujumbe wa shirika hilo uko njiani kuelekea kwenye kinu cha nyuklia cha Zaporizhia nchini Ukraine, kilicholengwa na mashambulizi katika wiki za hivi karibuni, hali iliyotia hofu ya kutokea kwa ajali kubwa

Kituo cha nyuklia cha Zaporizhia, karibu na Energodar, tarehe 22 Agosti 2022.
Kituo cha nyuklia cha Zaporizhia, karibu na Energodar, tarehe 22 Agosti 2022. REUTERS - ALEXANDER ERMOCHENKO
Matangazo ya kibiashara

"Siku imewadia, ujumbe wa IAEA kwenda Zaporizhia sasa uko njiani. Ni lazima tulinde usalama wa Ukraine na mtambo mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme barani Ulaya”, ameandika Rafael Grossi kwenye Twitter, akibainisha kuwa ujumbe huo utawasili kwenye eneo hilo"baadaye wiki hii". Katika picha iliyoambatana na ujumbe wake, mkuu wa IAEA akiwa katika picha ya pamoja na timu ya watu kumi, wakiwa wamevalia kofia na fulana zenye nembo ya shirika la Umoja wa Mataifa.

Rafael Grossi alikuwa ameomba kwa miezi kadhaa kuweza kwenda kwenye eneo la tukio, akionya juu ya "hatari halisi ya maafa ya nyuklia". Kiwanda cha Zaporizhia, ambapo kunapatikana vinu sita kati ya 15 vya Ukraine, kilidhibitiwa na wanajeshi wa Urusi mapema mwezi Machi, muda mfupi baada ya uvamizi dhidi ya Ukraine kuanza mnamo Februari 24, na kiko karibu na uwanja wa mapigano kusini mwa Ukraine.

Shutuma kutoka pande zote

Kyiv na Moscow wanatuhumiana kila mmoja kwa kufanya mashambulizi karibu na kituo hiki cha nyuklia, karibu na mji wa Energodar, kwenye Mto Dnieper, na hivyo kuweka kinu hiki katika hatari. Siku ya Jumamosi shirika la taifa la nishati ya nyuklia la Ukraine, Energoatom, lilionya juu ya hatari ya uvujaji wa mionzi na moto baada ya mashambuizi mapya. Katika wiki za hivi majuzi, nchi za magharibi zilitiwa wasiwasi na hali inayojiri karibu na kinu cha Zaporijgia. Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kukomeshwa kwa shughuli zote za kijeshi katika eneo lililokaribu na kituo hiki cha nyuklia.

Hapo awali, Ukraine ilihofia kuwa ziara kama hiyo ingehalalisha uvamizi wa Urusi kwenye kituo hicho mbele ya jumuiya ya kimataifa kabla ya hatimaye kuunga mkono wazo la ujumbe wa IAEA. Akikabiliwa na hali hii "hatari", Rais Volodymyr Zelensky alikuwa amewahimiza maafisa wa nyuklia wa Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa kutuma timu haraka iwezekanavyo.

Kati ya Alhamisi na Ijumaa, mtambo huo na vinu vyake sita vya megawati 1,000 kila kimoja "vilitenganishwa kabisa" na gridi ya taifa kutokana na kuharibika kwa njia za umeme, kulingana na Kyiv, kabla ya kuunganishwa na kuwashwa upya.

Vladimir Putin amekubali kwa ujumbe huo kwenda "Ukraine" na sio Urusi, madai ambayo ilikuwa imeyatoa hapo awali, ofisi ya rais wa Ufaransa ilikuwa imeonyesha katikati ya mwezi wa Agosti baada ya mahojiano ya simu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.