Pata taarifa kuu
SRI LANKA-SIASA

Sri Lanka: Hali yazidi kuwa kuwa tete licha ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu

Mzozo wa kisiasa unazidi kuwa mbaya nchini Sri Lanka. Jumatatu hii, Mei 9, baada ya mapigano makali kati ya wafuasi wa mamlaka na zafuasi wa upinzani, Waziri Mkuu Mahinda Rajapaksa alijiuzulu.

Mgogoro unazidi kuwa mbaya nchini Sri Lanka siku moja baada ya siku mbaya zaidi kushuhudiwa tangu kuanza kwa vuguvugu la maandamano. Hapa ni Colombo, Mei 10, 2022.
Mgogoro unazidi kuwa mbaya nchini Sri Lanka siku moja baada ya siku mbaya zaidi kushuhudiwa tangu kuanza kwa vuguvugu la maandamano. Hapa ni Colombo, Mei 10, 2022. AP - Eranga Jayawardena
Matangazo ya kibiashara

Kwa miezi kadhaa, kisiwa hicho kimekuwa kikikumbwa na mzozo ambao haujawahi kushuhudiwa, ukichochewa na janga la Covid-19 ambalo lilisababnisha nchi kupotewa fedha za kigeni kutoka kwa sekta ya utalii, na kuchochewa na safu ya maamuzi mabaya ya kisiasa, kulingana na wachumi. sheria ya kutotoka nje na isiyo na kikomo ilitangazwa na mamlaka.

Sri Lanka inatumbukia katika vurugu. Jeshi lilimhamisha Waziri Mkuu aliyejiuzulu Mahinda Rajapaksa kutoka kwa makazi yake rasmi huko Colombo leo Jumanne, Mei 10 kabla ya alfajiri, ili kumweka mahali salama baada ya maelfu ya waandamanaji kubomoa moja ya lango la jengo hilo.

"Baba yangu yuko salama, yuko mahali salama na anawasiliana na familia," mtoto wake, Namal Rajapaksa amesema. Mwanasheria huyo mwenye umri wa miaka 35, ndiye mzao ambaye uko wa familia ulikuwa umemtayarisha siku moja kuchukua mamlaka ya nchi. "Kuna uvumi ambao unasema kwamba tutaondoka. Hatutaondoka nchini”, amesisitiza, akitzjz hasira za waandamanajio dhidi ya familia yake kama "sura mbaya" kwa nchi.

Taifa hilo Kwa miezi kadhaa limekumbwa na ukosefu wa umeme, upungufu wa chakula, mafuta na chakula katika kile kinachosemekana kuwa hali mbaya zaidi  kuwahi kuikumbuka nchi hiyo tangu uhuru ilipojipatia uhuru wake hali iliyoaamsha maandamano dhidi ya serikali.

Msemaji wa Rajapaksa, Rohan Weliwita katika taarifa yake amesema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 76 ametuma barua ya kujiuzulu kwake kwa kaka yake mdogo Gotabaya Rajapaksa ambaye ni rais wa taifa hilo  hatua inayotoa nafasi ya kuundwa kwa serikali mpya.

"Ninajiuzulu haraka iwezekanavyo ilikukupa nafasi ya kuteua serikali inayojumuisha watu wote itakayosaidia taifa kutoka kwa mzozo wa sasa wa kiuchumi,” waziri mkuu huyo ameandika kwenye barua yake ya kujiuzulu.

Barua hii ya kujiuzulu kwa waziri mkuu wa Sri Lanka inamaana kuwa baraza la wabunge linapaswa kuvunjwa.

Chama kikuu cha upinzani nchini humo kabla ya maandamano kilikuwa kimesema kuwa hakitaingia katika serikali inayoongozwa na mtu wa jamii ya Rajapaksa.

Kumeshuhudiwa maandamano makubwa zaidi nchini humo siku ya jumatatu katika mji wa Colombo, hali iliyotokea baada ya wafuasi wanaounga mkono familia ya Rajapaksa kuwavamia waandamanji.

Zaidi ya watu 78 wamelazwa hosipitalini baada ya makabiliano hayo ambayo polisi wameayazima kwa kutumia mabomu ya machozi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.