Pata taarifa kuu

Sri Lanka: Sheria ya kutotoka nje yatangazwa baada ya machafuko

Polisi imetangaza marufuku ya kutotoka nje usiku kwa muda usiojulikana kuanzia Jumatatu (Mei 9) huko Colombo, mji mkuu wa Sri Lanka, kutokana na makabiliano kati ya wafuasi wa serikali na waandamanaji wanaomtaka Rais Gotabaya Rajapaksa ajiuzulu, shirika la habari la AFP limeandika.

Maandamano dhidi ya serikali ya Sri Lanka nje ya makazi ya Waziri Mkuu Mahinda Rajapaksa huko Colombo mnamo Aprili 24, 2022.
Maandamano dhidi ya serikali ya Sri Lanka nje ya makazi ya Waziri Mkuu Mahinda Rajapaksa huko Colombo mnamo Aprili 24, 2022. AP - Eranga Jayawardena
Matangazo ya kibiashara

Zoezi la upigaji kura linafanyika nchini Ufilipino, mamilioni ya raia wakiwa tayari wameoenekana wakipiga foleni wakiwa na nia ya kumchagua kiongozi wao mpya.

Ferdinand "Bongbong" Marcos Jr, mwanawe wa kiume wa diketea wa zamani kwenye taifa hilo akitarajiwa kuingia madarkani baada ya kura kupigwa kwenye taifa hilo.

Marcos Jr amepewa nafasi kubwa yakuibuka na ushindi mkubwa,  ushindi unaotarajiwa kurejesha madarakani uwongozi wa familia ya Marcos ulioangushwa miaka 36 iliyopita.

Mpinzani wa karibu wa Ferdinand "Bongbong" Marcos Jr ni Leni Rebredo aliyemshinda katika uchaguzi wa naibu rais wa mwaka wa 2016.

Vituo vya kupiga kura vimefunguliwa mapema saa kumi na mbili Afrika mashariki wapiga kura zaidi ya milioni 67 wakiwa tayari wameanza kupiga kura zao, maeneo ya shule yakiwa yanatumika kama vituo vya kupiga kura.

Licha ya zoezi hilo kuaanza mapema, baadhi ya vituo vya kupiga kura vimeripoti kukumbwa na changamoto kadhaa ikiwmo  kuweka makaratasi ya kura katika mashine ya kuhesabu kura,  wapiga kura wakitaka changamoto hiyo kushugulikiwa.

Maofisa wa polisi wameripoti kujeruhiwa kwa watu tisa katika shambulio la grenedi Kwenye eneo la Mindanao usalama ukiwa umeimarishwa kwa mujibu wa polisi.

Mshindi katika uchaguzi huu wa urais nchini Ufilipino, anatarajiwa kuchukua madaraka kutoka kwa Rodrigo Duterte,ambaye ameongoza taifa hilo kwa miaka sita.

Serikali ya rais Duterte imekuwa ikituhumiwa kwa kutumia nguvu zaidi wakati inapokuwa ikitekeleza operesheni ya kupiga vita matumizi ya mihadarati na ongezeko la uhalifu katika baadhi ya maeneo ya taifa hilo, madai ambayo utawala wake umejitenga nayo.

Bongbong Marcos, mwenye umri wa miaka 64, ni mtoto wa kiume wa dikteta za zamani nchini humo, Ferdinand Marcos, ambaye utawala wake ulidumu kwa miaka 21.

Tayari familia yake akiwemo mamake Imelda wamepiga kura katika kituo cha kupiga kura cha Batac kaskazini mwa taifa hilo eneo ambalo ndilo ngome yake ya kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.