Pata taarifa kuu

Maandamano yaendelea nchini Sri Lanka, Makataa ya kutembea nje yakitangazwa.

Polisi nchini Sri Lanka, imetangaza makataa ya watu kutembea nje hatua inayokuja baada ya wafuasi wanaoiunga mkono serikali na waandamanji kukabiliana wakitaka rais Gotabaya Rajapaksa kujiuzulu.

Mwandamanji aliyejeruhiwa katika maandamano nchini Sri Lanka.
Mwandamanji aliyejeruhiwa katika maandamano nchini Sri Lanka. AP - Eranga Jayawardena
Matangazo ya kibiashara

Karibia watu 20 wamejeruhiwa wakati wa makabiliano hayo kulingana na taarifa ya mamlaka kwenye taifa hilo.

Raia wanaomuunga mkono rais Rajapaksa, wameswashambulia kwa marungu watu waliokuwa wakiaandamana nje ya afisi yake wakimtaka kuondoka madarakani wakimtaja rais huyo kuwa kiongozi mbaya asiyejali mahitaji yao.  

Polisi wametumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya watu wanaounga serikali mkono ambao waliwazidi nguvu na kisha kuharibu mahema yaliokuwa yamesimikiwa na raia wanaoipinga serikali ya rais Gotabaya.

Shambulio hilo dhidi ya waandamanji limetokea ikiwa imepita siku moja baada ya waziri mkuu Mahinda Rajapaksa ambaye ni kaka yake rais Gotabaya kuzomewa na umma baaada yake kuonekana kwa mara ya kwanza tangu kuaanza kwa maandamano nchini humo.

Vyama vya wafanyikazi vimeanza maandamano ya kila wiki ya kushinikiza mabadiliko serikalini vyama hivyo vikimtaka pia rais kujiuzulu, Saman Rathnapriya mwanaharakati wa haki za wafanyikazi akisema zaidi ya vyama 1,000, vinavyowaakilisha wahudumu wa afya, bandari,elimu na wadau wengine muhimu wamejiunga na mchakato huo.

Sri Lanka imeendelea kupitia wakati mgumu wa kiuchumi hali ambayo imelitumbukiza taifa leo katika mzozo wa kisiasa, maandamano yakionekana kushika kasi nchini humo.

Kwa miezi kadhaa sasa, raia kwenye taifa hilo wameonekana wakipanga foleni ndefu kununua mafuta, gesi ya kupika, chakula na dawa,  bidhaa hizi muhimu zikitoka nje ya nchi.

Licha ya maandamano haya, familia ya Rajapaksa, akiwemo rais na waziri mkuu wamekataa  kuitikia wito wa kujiuzulu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.