Pata taarifa kuu

Waziri mkuu wa Sri Lanka Mahinda Rajapaksa amejiuzulu baada ya maandamano .

Waziri mkuu wa Sri Lanka, Mahinda Rajapaksa, amejiuzulu kutoka Kwa wadhifa wake hatua inayokuja baada ya mamia ya raia kulazwa hosipitalini baada ya wafuasi wake waliokuwa wamejihami kwa rungu kuwashambulia waandamanji.

 Waziri Mkuu wa Sri Lanka, Mahinda Rajapaksa
Waziri Mkuu wa Sri Lanka, Mahinda Rajapaksa © AFP
Matangazo ya kibiashara

Taifa hilo Kwa miezi kadhaa limekumbwa na ukosefu wa umeme, upungufu wa chakula, mafuta na chakula katika kile kinachosemekana kuwa hali mbaya zaidi  kuwahi kuikumbuka nchi hiyo tangu uhuru ilipojipatia uhuru wake hali iliyoaamsha maandamano dhidi ya serikali.

Msemaji wa Rajapaksa, Rohan Weliwita katika taarifa yake amesema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 76 ametuma barua ya kujiuzulu kwake kwa kaka yake mdogo Gotabaya Rajapaksa ambaye ni rais wa taifa hilo  hatua inayotoa nafasi ya kuundwa kwa serikali mpya.

"Ninajiuzulu haraka iwezekanavyo ilikukupa nafasi ya kuteua serikali inayojumuisha watu wote itakayosaidia taifa kutoka kwa mzozo wa sasa wa kiuchumi,” waziri mkuu huyo ameandika kwenye barua yake ya kujiuzulu.

Barua hii ya kujiuzulu kwa waziri mkuu wa Sri Lanka inamaana kuwa baraza la wabunge linapaswa kuvunjwa.

Chama kikuu cha upinzani nchini humo kabla ya maandamano kilikuwa kimesema kuwa hakitaingia katika serikali inayoongozwa na mtu wa jamii ya Rajapaksa.

Kumeshuhudiwa maandamano makubwa zaidi nchini humo siku ya jumatatu katika mji wa Colombo, hali iliyotokea baada ya wafuasi wanaounga mkono familia ya Rajapaksa kuwavamia waandamanji.

Zaidi ya watu 78 wamelazwa hosipitalini baada ya makabiliano hayo ambayo polisi wameayazima kwa kutumia mabomu ya machozi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.