Pata taarifa kuu

Covid-19 Austria: Chanjo ya lazima kwa watu wazima kuanzia Februari

Baada ya wiki chache, chanjo ya watu wazima itakuwa ya lazima nchini Austria. Kuanzia mwanzoni mwa mwezi wa Februari, wale ambao hawajachanjwa watatozwa faini kubwa. Tangazo hili lilitolewa Jumapili hii, Januari 16, na Kansela wa Austria, Karl Nehammer.

Chanjo kwa watu wazima itakuwa ya lazima nchini Austria kuanzia Februari 2022.
Chanjo kwa watu wazima itakuwa ya lazima nchini Austria kuanzia Februari 2022. Damien MEYER AFP/File
Matangazo ya kibiashara

"Tutapitisha wajibu wa chanjo kama ilivyopangwa. Itaanza kutumika mwanzoni mwa mwezi wa Februari. Kwa uhakika hili ni suala nyeti sana. Ili kuchukua hatua hii, unapaswa kuzingatia mambo mengi ... Na ndivyo tulivyofanya. Kwa hivyo, chanjo ya lazima itaanza kutumika mwanzoni mwa mwezi wa Februari, " amesema Kansela wa Austria. Watu 27,000 bado waliandamana Jumamosi Januari 16 katika mji mkuu wa Austria kupinga hatua hii tata, inayoshutumiwa kwa kukiuka uhuru wa mtu binafsi.

"Itaanza na awamu ya awali ambapo watu watapata fursa ya kupata chanjo, ili kuweza kushawishika. Awamu ambayo itakuwa kama ya kuleta matumaini, amebaini Karl Nehammer.

Faini ya hadi euro 3,600

Wote ambao hawajachanjwa watapokea wito wa kuchomwa sindano ya kwanza na wale ambao hawatajitokeza watatozwa faini baada ya kukumbushwa. Sheria inatoa hadi faini nne kwa kila mtu. Polisi watapewa uwezo wa kufanya ukaguzi kwenye barabara kuu.

"Baada ya awamu hii ya kukabiliana, ambayo itamalizika katikati ya mwezi wa Machi, chanjo itafanyiwa ukaguzi. Na kutoweza kuwasilisha kibali cha chanjo kwa wakaguzi itakuwa kosa,” ameonya Kansela. Kosa hili litaadhibiwa kwa adhabu ya kuanzia euro 600 hadi 3,600 iwapo kuna kosa la kurudia. Sheria hiyo imepangwa kutumika hadi Januari 31, 2024.

Serikali ya Austria inatetea hatua hii kwa kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa katika hospitali mbalimbali kutokana na maambukizi ya kirusi kipya cha ya Omicron na nia yake ya kufikia kiwango cha chanjo cha 90%, kuwezesha, kulingana na ushauri wa wataalam wake, kufikia kinga ya pamoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.