Pata taarifa kuu

Austria yakabiliwa na mlipuko mpya wa COVID-19

Nchi ya Austria inatarajiwa kurejesha tena hali ya watu kutotembea nje kufuatia kupanda tena kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

Wazazi wakiwa na watoto wao wanafika katika kituo cha chanjo ya Covid-19 huko Vienna.
Wazazi wakiwa na watoto wao wanafika katika kituo cha chanjo ya Covid-19 huko Vienna. © AFP - JOE KLAMAR
Matangazo ya kibiashara

Taifa hilo linalopatikana Magharibi mwa Ulaya, linakuwa taifa la kwanza katika eneo hilo kuchukua hatua hii baada ya kuripoti kwa mlipuko mpya wa virusi vya Covid-19 nchini humo.

Kuanzia siku ya Jumatatu watu ambao hawajapata chanjo, hawataruhusiwa kutembea nje, wakati huu ikilenga kuwachanja raia wake wote ifikapo mwezi Februari mwaka 2022.

Nchi hiyo imerekodi idadi kubwa ya maambukizi barani Afrika, huku watu 991 kati ya Laki Moja wanaofanyiwa vipimo, wakipatikana wameambukizwa kwa kipindi cha siku saba zilizopita.

Mikoa iliyoathirika zaidi ni Salzburg na  Austria Kasazini. Kiongozi wa nchi hiyo Kansela Alexander Schallenberg amesema, mpaka sasa serikali hiyo haijafanikiwa kuwashawishi watu kukubali kupata chanjo.

Aidha, amesema watu nchini humo wanaokataa kupokea chanjo ndio wanaosababisha kuongezeka kwa maambukizi hayo aliyosema ni shambulizi katika sekta ya afya.

Mpaka sasa ni thuluthi mbili ya raia wa Austria ndio waliopata chanjo kamili ya kuzuia maambukizi ya Covid-19 wakati huu kipindi cha baridi kikikaribia barani Ulaya, na watalaam wanashauri nchi mbalimbali kuanza kufikiria kurejesha masharti ya watu kutotembea katika maeneo muhimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.