Pata taarifa kuu
EU-POLAND-HUNGARY-UCHUMI

Bajeti ya Ulaya: Poland yasubiri mapendekezo kutoka Brussels

Poland, ambayo kama Hungary imezuia rasimu ya bajeti ya Umoja wa Ulaya, inatarajia Brussels kutoa mapendekezo mapya ili kuondokana na sintofahamu inayojiri wakati huu kati ya pande hizo mbili, msemaji wa serikali ya Poland amesema leo Jumanne.

Kikao cha viongozi wa Umoja wa Ulaya huko Brussels.
Kikao cha viongozi wa Umoja wa Ulaya huko Brussels. REUTERS/Piroschka van de Wouw/Pool
Matangazo ya kibiashara

"Tunasubiri mapendekezo mapya kulingana na makubaliano ya Umoja wa Ulaya na hitimisho la Baraza la Ulaya la mwezi Julai, ambapo bajeti ya umoja huo iliidhinishwa," msemaji wa serikali ya Poland amesema kwenye kituo cha redio ya umma.

Rasimu ya bajeti ya Umoja wa Ulaya kwa kipindi cha 2021-2027, ambayo ni sawa na euro trilioni 1.1, inaambatana na euro bilioni 750 za kufufua uchumi.

Budapest na Warsaw wanapinga vikali kuanzishwa masharti ya kutolewa kwa fedha za bajeti za Umoja wa Ulaya na wamedai kuwa walizuia majaribio kadhaa ya kutungwa kanuni za aina hiyo kwenye mkutano wa kilele wa kanda hiyo mwezi Julai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.