Pata taarifa kuu
EU-UINGEREZA-USHIRIKIANO

Brexit: Siku saba hadi 10 kufikia makubaliano kati ya Brussels na London

Waziri wa Mambo ya nje wa Ireland amebaini leo Jumatatu kwamba Umoja wa Ulaya na Uingereza bado wana siku karibu kumi kufikia makubaliano juu ya uhusiano wao wa baadaye kwani kila upande unataka mwingine kulegeza msimamo wake juu ya uvuvi na sheria za ushindani sawa.

Baada ya kushindwa kuhitimisha makubaliano kwenye tarehe ya mwisho ya mwezi Novemba, London na Brussels zimeanza tena mazungumzo yao leo Jumatatu.
Baada ya kushindwa kuhitimisha makubaliano kwenye tarehe ya mwisho ya mwezi Novemba, London na Brussels zimeanza tena mazungumzo yao leo Jumatatu. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Kwa kweli tuko katika wiki ya mwisho(...), ikiwa hakutapatikana maendeleo makubwa wiki ijayo, ndani ya siku 10, nadhani tutakuwa katika matatizo makubwa na lengo litakuwa kujiandaa kwa 'Uingereza kujitoa bila ya mkataba' na kukubali athari zote zitakazotokea, "Simon Coveney amesema kwenye redio ya Ireland Newstalk.

"Nadhani serikali ya Uingereza inajua vizuri kile kinachotakiwa kufanywa ili kufanikisha makubaliano wiki hii, swali la kweli ni kujuwa ikiwa ina nia ya kisiasa ya kulifanya. Nadhani tutapata mkataba, ni ubashiri wangu kwa muda mrefu, lakini sitashangaa ikiwa itashindikana, ”Simon Coveney ameongeza.

Baada ya kushindwa kuhitimisha makubaliano kwenye tarehe ya mwisho ya mwezi Novemba, London na Brussels zimeanza tena mazungumzo yao leo Jumatatu.

Pande zote mbili bado zinasema zinataka kufikia makubaliano ifikapo Desemba 31, tarehe ya kumalizika kwa kipindi cha mpito kufuatia Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, EU.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.