Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO

Brexit: Mazungumzo yaanza tena London, baada ya kukwama kwa wiki moja

Baada ya wiki moja ya mkwamo, Uingereza na Umoja wa Ulaya wanaanza tena mazungumzo yao ya kibiashara ya baada ya Brexit huko London leo Alhamisi, pamoja na kutafutia ufumbuzi tofauti kubwa zilizopo wakati kukisalia muda mdogo ili kuepuka Uingereza kujiondoa bila ya mkataba.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson katika mbele ya Baraza la Wawakilishi huko London, Oktoba 21, 2020.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson katika mbele ya Baraza la Wawakilishi huko London, Oktoba 21, 2020. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Ni wazi, tofauti kubwa imebaki kati ya msimamo wetu juu ya masuala magumu zaidi, lakini tuko tayari na Umoja wa Ulaya kuona ikiwa inawezekana kuzileta pamoja katika mazungumzo hayo," amesema msemaji wa Waziri Mkuu Boris Johnson katika taarifa. "Inawezekana mazungumzo hakafeli," ameonya.

Umoja wa Ulaya umeonya kwamba maelewano lazima yapatikane kabla ya mwisho wa mwezi wa Oktoba ili makubaliano ya biashara huria yawepo Januari 1, tarehe ambayo kitakuwa kimemalizika kipindi cha mpito wakati ambapo sheria za Ulaya zitakuwa zikiendelea kutumika katika ardhi ya UIngereza.

Mjumbe wa Umoja wa Ulaya Michel Barnier amesema kuwa Ulaya iko tayari kuchukua hatua ya kuukwamua mkwamo wa Brexit, matamshi ambayo yamekaribishwa na Uingereza na kuongeza matumaini kuwa mazungumzo hayo yatakwamuliwa.

Barnier amekiambia kikao cha Bunge la Ulaya mjini Brussels kuwa anahisi makubaliano yako karibu, kama pande zote zipo tayari kushirikiana na kuonyesha dhamira ya kufikia makubaliano.

Uingereza ilisitisha kwa ghafla mazungumzo hayo baada ya viongozi wa Umoja wa Ulaya katika mkutano wa kilele kusema kuwa sasa mpira upo uwanjani mwa Uingereza na sio Umoja wa Ulaya kufikia makubaliano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.