Pata taarifa kuu
UFARANSA-UTURUKI-UGIRIKI-USHIRIKIANO

Paris yaitaka Ankara kutekeleza ahadi zake kwenye bahari ya Mediterania

Paris inasubiri Uturuki kutekeleza ahadi zake, kujiepusha na chokochoko zaidi na kutoa ahadi halisi za utayari wake wa kushiriki mazungumzo kwa nia njema, msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya Ufaransa imesema leo Jumatatu kuhusiana na mzozo kati ya Athenes na Ankara mashariki mwa Mediterania.

Meli ya Uturuki inayofanya utafiti wa utafutaji wa gesi katika eneo la bahari ya Mediterania,Oruc Reis katika maji ya Bosphore huko Istambul, Oktoba 3, 2018.
Meli ya Uturuki inayofanya utafiti wa utafutaji wa gesi katika eneo la bahari ya Mediterania,Oruc Reis katika maji ya Bosphore huko Istambul, Oktoba 3, 2018. Semih Ersozler/DHA via AP
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa ina wasiwasi juu ya tangazo la Uturuki la kutuma tena meli yake iliyokuwa inafanya utafiti wa utafutaji wa gesi katika eneo la bahari ya Mediterania, Oruc Reis, ameongeza Agnès von der Mühll.

Meli ya Uturuki ya Oruç Reis, iliyotumwa Jumatatu wiki hii, inatarajia kutekeleza kazi yake Kusini mwa kisiwa cha Ugiriki cha Kastellorizo, karibu na pwani ya kusini mwa Uturuki, kulingana na hati ya baharini iliyochapishwa Jumapili jioni.

Ugiriki imeuita uamuzi wa Uturuki wa kutuma meli yake katika eneo la mashariki mwa Mediterania, eneo lenye utajiri mkubwa wa rasilimali za mafuta na gesi , kama "kuongezeka kwa uchokozi" unaotishia amani ya kanda nzima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.