Pata taarifa kuu
UTURUKI-UGIRIKI-USALAMA-USHIRIKIANO

Uturuki yairejesha meli yake mashariki mwa Mediterania

Meli ya Uturuki iliyokuwa inafanya utafiti wa utafutaji wa gesi katika eneo la bahari ya Mediterania, Oruc Reis, ambayo imesababisha hali ya kuzorota kwa mahusiano kati ya serikali za Uturuki na Ugiriki, imerejeshwa katika eneo hilo Jumatatu hii, Oktoba 12.

Meli ya Uturuki inayofanya utafiti wa utafutaji wa gesi katika eneo la bahari ya Mediterania,Oruc Reis katika maji ya Bosphore huko Istambul, Oktoba 3, 2018.
Meli ya Uturuki inayofanya utafiti wa utafutaji wa gesi katika eneo la bahari ya Mediterania,Oruc Reis katika maji ya Bosphore huko Istambul, Oktoba 3, 2018. REUTERS/Yoruk Isik
Matangazo ya kibiashara

Meli ya Oruc Reis imerejeshwa katika eneo iliyokupo mwezi Septemba huko Mashariki mwa Mediterania, kikosi cha wanamlaji cha Uturuki kimebaini.

Kurejea kwa meli ya Oruc Reis katika eneo linalozozaniwa la bahari ya Mediterania, kunaweza kuzidisha mvutano kati ya Uturuki na Ugiriki.

Athenes na Ankara ziliingia katika mvutano mkubwa uliodumu mwezi mmoja baada ya Uturuki kutuma meli hiyo, ikisindikizwa na meli za kivita, katika eneo lenye utajiri wa gesi asilia, linalodaiwa na Ugiriki kuwa ni sehemu yake.

Taarifa ya kurejea kwa meli ya Oruc Reis Mashariki mwa Mediterania, pamoja na kusini mwa kisiwa cha Uigiriki cha Kastellorizo, kilomita mbili kutoka pwani ya Uturuki, kuna hatari ya kutafsirika, huko Athenes sawa na Brussels, kama chokochoko kutoka Ankara.

Uturuki na Ugiriki, zote zikiwa wanachama wa jumuiya ya kujihami ya NATO, zinazozana kuhusu haki juu ya rasilimali za mafuta na gesi inayodhaniwa kuwepo katika eneo la Mashariki mwa bahari ya Mediterania, kwa msingi wa madai kinzani juu ya ukubwa wa miambao yao ya bara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.