Pata taarifa kuu
UJERUMANI-UFARANSA-EU-CORONA-UCHUMI

Paris na Berlin wapendekeza mpango wa euro bilioni 500 kunusuru uchumi wa Ulaya

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wamependekeza kuanzishwa kwa mfuko wa euro bilioni 500 wa kufadhili juhudi za kuukwamua uchumi wa nchi za Ulaya zilizoathirika zaidi na janga la Corona.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wakati wa mkutano kupitia video Mei 18, 2020.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wakati wa mkutano kupitia video Mei 18, 2020. Kay NIETFELD / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa wawili hao mpango huo sasa unaandaliwa jijini nchini Ubelgiji na nchi zitakazonufaika ni zile ambazo shughuli za kiuchumi zimezorota katika bara hilo kutokana na janga la Corona.

Pendekezo hilo linaashiria mabadiliko katika msimamo wa Ujerumani.

Mpango huu wa pamoja, ambao bado haujaidhinishwa na Tume ya Ulaya na nchi 27 wanachama wa umoja huo, ni "hatua kubwa" na "mabadiliko ya falsafa", amekaribisha Emmanuel Macron wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano na mwenzake wa Ujerumani Angela Merkel kupitia video Jumatatu Mei 18.

Taarifa ya viongozi hao wawili imesema kuwa fedha hizo zitakazotolewa kupitia ufadhili wa mikopo kwa niaba ya Umoja wa Ulaya, zitapelekwa kwa sekta na maeneo ya umoja huo ambayo yameathirika pakubwa.

"Kwa mara ya kwanza, kile tunachopendekeza pamoja, Ujerumani na Ufaransa, ni kuamua sote kwa pamoja kwenda kufuta deni la pamoja kwenye masoko na kutumia euro bilioni 500, deni ambalo litalipwa, kwa kusaidi kifedha sekta zilizoathirika zaidi na kwa maeneo yaliyoathiriwa zaidi, na kwa hivyo kukubali mkakati halisi wa pamoja, "amesisitiza Emmanuel Macron.

Merkel amesema kuwa wana uhakika kuwa sio haki tu bali pia ni muhimu kuzitoa fedha hizo, ambazo baadae zitarejeshwa pole pole kupitia bajeti kadhaa za siku za usoni za Ulaya. Macron ameongeza kuwa nchi zitakazonufaika na ufadhili huo hazitahitaji kurudisha fedha hizo, akisisitiza kuwa sio mikopo.

Rais wa Halmashauri kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen ambaye anatarajiwa kusaidia katika utekelezaji wake, ameyasifu mapendekezo ya mpango huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.