Pata taarifa kuu

Coronavirus-duniani: Hali kuhusu janga la Corona Jumatano Mei 13

Janga la coronavirus limesababisha vifo vya watu wasiopungua 292,000 na watu zaidi ya milioni 4 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona duniani.

Brussels, Ubelgiji, Aprili 16, 2020. Baada ya biashara kufungua tena wiki hii, shule zitaanza kuwapokea tena wanafunzi Jumatatu Mei 18.
Brussels, Ubelgiji, Aprili 16, 2020. Baada ya biashara kufungua tena wiki hii, shule zitaanza kuwapokea tena wanafunzi Jumatatu Mei 18. REUTERS/Francois Lenoir/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Ulaya ambayo tangu mapema wiki hii ilianza kulegeza vizuizi vya kudhibiti ugonjwa huo, imetoa wito wa kuanza tena kufungua mipaka kadri hali inavyokuwa.

Zoezi la kulegeza vizuizi vya kudhibiti ugonjwa wa Covid linaendelea nchini Ufaransa wakati shule kashaa zimeanza shughuli zao za kawaida. Baadhi ya sehemu za starehe zimefunguliwa tena Jumatano wiki hii wakati manispaa ya jiji la Paris likitangaza kwamba maeneo yanayotembelewa na watu wengi katika mji mkuu wa nchi hiyo yataendelea kufungwa. Siku tatu baada ya kumalizika kwa marufuku ya kutotembea, "ni mapema sana kutangaza ushindi" lakini njia iliyofuatwa "ndio inayofaa", rais Emmanuel Macron amebaini wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la Mawaziri, akinukuliwa na msemaji wa serikali.

Watu 27,000 wamefariki dunia nchini Ufaransa kutokana na janga la Corona, baada ya kuripotiwa vifo vipya 83 ndani ya saa 24, lakini idadi ya wagonjwa inaendelea kupungua, kulingana na ripoti ya mamlaka ya ya afya Jumatano jioni. Ugonjwa wa Covid-19 umeua watu 27,074 tangu Machi 1, lakini shinikizo kwenye huduma za dharura linaendelea kupungua, kwa wagonjwa walio chini ya 2,500 (sawa na 2,428) kwa mara ya kwanza tangu Machi 24, na chini ya wagonjwa 114 Jumanne, wiki hii, mamlaka ya afya nchini Ufaransa imesema.

Wakati huo huo mataifa kadhaa ya Ulaya ikiwemo Ujerumani, Austria na Uswisi zimetangaza mipango ya kulegeza masharti ya udhibiti wa mipakani kuazia katikati ya mwezi Juni, wakati bodi tendaji ya Umoja wa Ulaya ikitoa muongozo wa usalama katika kipindi cha kiangazi.

Naye Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte ametangaza uwasilishaji wa kitita cha dola bilioni 59.5 kwa ajili ya hatua ya kuanza ufufuzi wa uchumi na kuwasaidia wanachi katika taifa hilo ambalo ni miongoni mwa mataifa yaliotahiriwa vibaya kabisa na mripuko wa virusi vyacoronaduniani. Rekodi za sasa zinaonesha taifa hilo lina vifo 31,000.

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika ya Kusini amesema ana lengo la kuendelea kuondosha vizuizi zaidi vilivyowekwa katika kukabiliana na janga la virusi vya corona lakini katika maeneo ambayo yameathiriwa zaidi, vitaendelea kuwepo hadi Juni.

China imeripoti visa vitatu vya maambukizi ya virusi vya corona, ikiwa ni pungufu ya visa saba vilivyorekodiwa siku moja kabla. Wizara ya Afya ya China imesema visa vyote hivyo vimetokana na maambukizi ya ndani. Idadi ya maambukizi kwa sasa imefikia watu 82,929 wakati vifo vimesalia kuwa 4,633.

Wizara ya Afya ya Brazil imetoa takwimu zinazoonesha maambukizi mapya 11,385 ya virusi vya corona, pamoja na vifo 749 kwa siku. Hadi sasa taifa hilo lina idadi ya maambukizi 188,974, tangu kuanza kwa mripuko huko likiipita Ufaransa yenye maambukizi 177,700. Na kwa hali ilivyo nchini Brazil inabashiria kuwa taifa la sita litakaloathiriwa vikali duniani.

Marekani imeanza kaunzishwa upya uchumi wake baada ya miezi kadhaa ya mkwamo uliosababishwa na vizuizi vya kukabiliana na virusi vya corona, lakini wachambuzi wanasema itaweza kuchukua muda wa majuma kadhaa hadi kufahamika wazi kwamba, biashara zinazofunguliwa zitasababisha kupanga kwa maambukizi. Marekani ina maambukizi zaidi ya watu milioni 1.4 na vifo zaidi ya elfu 80.

Hata hivyo Shirika la Afya Duniani limesema huenda virusi vya corona visiishe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.