Pata taarifa kuu
DUNIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Wabunge watoa wito wa kufuta madeni kwa nchi masikini

Zaidi ya wabunge 300 kutoka nchi ishirini wametoa wito leo Jumatano kwa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia kufuta madeni kwa nchi masikini zinazokabiliwa na athari za kiuchumi zinazotokana na janga la Corona.

Nchi nyingi masikini zinakabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni kutoka Shirika la fedha la Kimataifa na Benki Kuu ya Duna.
Nchi nyingi masikini zinakabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni kutoka Shirika la fedha la Kimataifa na Benki Kuu ya Duna. REUTERS/Yuri Gripas/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Seneta wa Marekani Bernie Sanders, mmoja wa waasisi wa mpango huo pamoja na mbunge kutoka Chama cha Democratic Ilhan Omar, amesema nchi masikini lazima ziweze kuonyesha udhaifu wa rasilimali zao zote ili kulinda raia wao badala ya kulipa mzigo mkubwa wa "madeni yasiyowezekana" kutoka kwa taasisi kuu za kifedha za kimataifa.

Msamaha wa madeni kwa nchi masikini ni "kidogo zaidi ya mambo ambayo Benki ya Dunia, IMF na taasisi zingine za kifedha za kimataifa zinapaswa kufanya ili kuzuia kuongezeka kwa umaskini, njaa na magonjwa ambayo yanatishia mamia ya mamilioni ya watu, "amesema.

Nchi mbalimbali zinabaini kwamba ulipaji wa madeni kwa nchi masikini zaidi unapaswa kufutwa kabisa badala ya kusitishwa tu, kama zilivyoamua nchi zilizoendelea kiviwanda na zinazoinukia kwa kasi kiuchumi G20 mnamo mwezi wa Aprili mwaka huu.

Benki ya Dunia imesema itafikiria njia za kuongeza usaidizi kwa nchi masikini zaidi, lakini kufutwa kwa madeni kwa nchi hizo kunaweza kuathiri kiwango chake cha mkopo na kupunguza uwezo wake wa kutoa fedha za kiwango cha chini kwa wanachama wake.

Wabunge waliotia saini kwenye waraka huo ni pamoja na Jeremy Corbyn na kiongozi wazamani wa Argentina Carlos Menem.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.