Pata taarifa kuu
UFARANSA-ULAYA-CORONA-AFYA

Ufaransa yawarudisha nyumbani raia zaidi ya 150 wa Ulaya kutoka Panama

Zaidi ya raia 150 kutoka matiafa mbalimbali ya Ulaya waliokuwa wamekwama nchini Panama na Honduras wamerejeshwa nyumbani tangu Jumatatu wiki hii nchini Ufaransa, wakati nchi nyingi barani Ulaya zilianza tangu Jumatatu wiki hii kulegeza vizuizi vya kudhibiti ugonjwa wa Covid-19.

Ufaransa imewarejesha makwao baadhi ya raia kutoka Ulaya waliokuwa wamekwama nchini Panama.
Ufaransa imewarejesha makwao baadhi ya raia kutoka Ulaya waliokuwa wamekwama nchini Panama. AFP PHOTO / Rodrigo ARANGUA
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Ufaransa inatarajia kuwarudisha raia wengine wa Ulaya Jumatano wiki hii.

Balozi wa Ufaransa nchini Panama, Brice Roquefeuil, amepongeza "juhudi kubwa za uratibu" pamoja na washirika wake katika Umoja wa Ulaya kusafirisha raia 59 wa Ufaransa, 27 kutoka Uhispania, Wajerumani 18, raia 12 kutoka Italia na 10 kutoka Uholanzi, miongoni mwa mataifa mengine yaliyowakilishwa.

Wakati huo huo katika nchi kadhaa za Ulaya, wanafunzi na walimu waliripoti shuleni Jumatatu wiki hii, baada ya wiki kadhaa wakitakiwa kubaki ndani katika juhudi za kudhibiti maambukizi ya ugonjwa hatari wa Covid-19.

Nchini Italia imetangaza kwamba wanafunzi watarejea shuleni kabla ya mwezi kabla ya Septemba mwaka huu.

Hata hivyo Shirika la Afya Duniani, WHO, limeonya kuhusu kutokea kwa wimbi la pili la mlipuko wa corona iwapo hakutachukuliwa hatua kali za kukabiliana na ugonjwa huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.