Pata taarifa kuu
UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Ujerumani yajiandaa kwa wimbi la pili la maambukizi zaidi

Shughuli za ujenzi katika kituo cha maonyesho katika mji mkuu wa Ujrumani, Berlin, zinaendelea kwa kusubiri wagonjwa zaidi licha ya kuwa nchi hiyo imeweka marufuku ya kutembea.

Hospitali inayohudumia wagonjwa wa Corona iliyoanzishwa katika Kituo cha Maonyesho cha Berlin, picha iliyopigwa Aprili 23, 2020.
Hospitali inayohudumia wagonjwa wa Corona iliyoanzishwa katika Kituo cha Maonyesho cha Berlin, picha iliyopigwa Aprili 23, 2020. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Vyumba vikubwa visivyo na kitu vinatarajiwa kuwa hospitali katika wiki chache zijazo.

Hivi karibuni Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alielezea hofu yake ya kutokea wimbi kubwa na wagonjwa aw Covd-19 nchini humo.

Kuna "hatari ya msingi" ambayo ni kuwa maambukizi yanaweza kurejea tena "ikiwa vizuizi vya kupambana dhidi ya Covid-19 vitaondolewa mapema," alisema siku ay Jumanne Lars Schaade, mkurugenzi msaidizi wa chuo kikuu cha Marekani cha Robert Koch, taasisi inayohusika na udhibiti wa magonjwa.

Katika hospitali ya chuo kikuu cha Aachen, ambacho kilipokea visa vikuu vya kwanza vya Covid-19 nchini Ujerumani, vitanda kadhaa bado viko tupu kwa kusubiri wagonjwa zaidi.

Hivi karibuni Shirika la Afya Duniani, WHO, lilisema nusu ya vifo vilivyotokea barani Ulaya kutokana na virusi vya Corona vilikuwa katika nyumba za kuwaangalia wazee.  

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.