Pata taarifa kuu
UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa zaidi ya 100,000 vya maambukizi vyathibitishwa Ujerumani

Watu 103,228 wameambukiwza virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19, ambao umesababisha vifo 1,861 nchini Ujerumani, kuli,ngana na takwimu iliyotolewa Jumatano na Taasisi ya Robert Koch (RKI) inayohusika na masuala ya magonjwa ya kuambukia.

Hatimaye Ujerumani inafanya vipimo 500,000 kwa wiki kujua hali ya raia kutokana na janga la Covid-19.
Hatimaye Ujerumani inafanya vipimo 500,000 kwa wiki kujua hali ya raia kutokana na janga la Covid-19. REUTERS/Axel Schmidt
Matangazo ya kibiashara

Hii inaonyesha visa vipya 4,003 vya maambukizi na vifo vipya 254 kwa siku moja, kulingana na ripoti ya RKI.

Ugonjwa wa Covid-19 unaendelea kuathiri nchi mbalimbali duniani, huku maambukizi ya ugonjwa huo duniani yakifikia milioni moja, huku watu wakiendelea kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

Idadi ya visa vya maambukizi vilivyothibitishwa ulimwenguni inazidi milioni moja, huku watu zaidi 52,000 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa Covid-19, kulingana na takwimu zilizotolewa na shirika la habari la AFP.

Ulaya ndio bara lililoathiriwa zaidi, lakini Marekani inaelekea kuwa kitovu kipya cha janga hilo, ikiripoti robo ya visa vya maambukizi. Idadi hii labda ni ndogo, kwa sababu ya ukosefu wa uchunguzi wa kutosha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.