Pata taarifa kuu
AFRIKA-IMF-CORONA-AFYA

Benki ya Dunia na IMF zaombwa kusaidia nchi za Afrika katika vita dhidi ya Corona

Mashirika zaidi ya 140 yasiyokuwa ya kiserikali barani Afrika, yanataka mashirika ya kimataifa kama Shirika la Fedha Duniani, IMF, na Benki ya dunia, kuyasaidia mataifa ya Afrika kupambana na maambukizi ya Corona.

Nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na ugonjwa wa Covid-19.
Nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na ugonjwa wa Covid-19. tv360nigeria
Matangazo ya kibiashara

Wito huu umekuja kipindi hiki ambacho pia, mataifa tajiri yaliombwa pia kusemehe madeni kwa mataifa masikini barani Afrika yanapoendelea kupambana na virusi vya Corona.

Waziri wa fedha nchini Ghana, Ken Ofori Atta, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati inayoshauri Benki ya Dunia na IMF, ameitaka China kuwa katika mstari wa mbele kutangaza msamaha wa madeni kwa mataifa ya Afrika.

Mataifa 69 mengi yakiwa barani Afrika, yanadaiwa na mataifa tajiri pamoja na wakopeshaji binafasi zaidia ya Dola za Marekani Bilioni 25.

Wakati huo huo, Shirika la Fedha Duniani, IMF, linasema kuwa linatoa Dola Bilioni 50 kuyasaidia mataifa zaidi ya 80 ambayo yameomba msaada wa fedha, huku Benki ya Dunia ikitoa Dola Bilioni  14 kusaidia katika vita dhidi ya virusi vya Corona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.