Pata taarifa kuu
UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya visa vya maambukizi yaongezeka Ujerumani

Idadi ya visa vipya vya maambukizi ya virusi vya Corona vilivyothibitishwa imeongezeka kwa visa 1,785 katika masaa 24 yaliyopita nchini Ujerumani, kulingana na takwimu iliyotolewa Jumanne na Chuo Kikuu cha Robert Koch (RKI).

Wateja wa kwanza tangu kufunguliwa kwa baadhi ya maduka nchini Ujerumani Aprili 20, 2020.
Wateja wa kwanza tangu kufunguliwa kwa baadhi ya maduka nchini Ujerumani Aprili 20, 2020. REUTERS/Ralph Orlowski
Matangazo ya kibiashara

Ripoti iliyotolewa Jumatatu ilibaini visa vipya 1,775 vya maambukizi ya virusi vya Corona.

Jumla ya visa 143,457 vya maambukizi vimeripotiwa tangu kuzuka kwa janga la Covid-19 nchini Ujerumani.

Kuhusu idadi ya vifo vinavyotokana na virusi vya Corona, imeongezeka kutoka 194 jana Jumatatu hadi 4.598 leo Jumanne, kwa mujibu wa shirika la habri la Reuters.

Hata hivyo baadhi ya miji katika nchi zilizoathiriwa vibaya na janga la Corona barani Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ujerumani, imeanza kufungua baadhi ya biashara na huduma, baada ya kuzifunga kwa muda tangu kuiingia kwa janga hilo barani humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.