Pata taarifa kuu
UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya vifo yaongezeka Ujerumani

Watu 67,366 tayari wameambukizwa virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19 nchini Ujrumani na watu 732 wamefariki dunia kwa ugonjwa huo, kulingana na ripoti iliyotolewa leo Jumatano na mamlaka ya afya nchini humo, Robert Koch (RKI).

Hatimaye Ujerumani inafanya vipimo 500,000 kwa wiki kujua hali ya raia kutokana na janga la Covid-19.
Hatimaye Ujerumani inafanya vipimo 500,000 kwa wiki kujua hali ya raia kutokana na janga la Covid-19. REUTERS/Axel Schmidt
Matangazo ya kibiashara

Hii inaonyesha visa vipya 5,453 vya maambukizi na vifo vipya zaidi ya 149 kwa siku moja, kulingana na ripoti ya RKI.

Hayo yanajiri wakati shirika la afya Duniani, WHO, limeonya kuwa janga hilo halijamalizika katika mataifa ya Asia.

Wakati huo huo vifo kutokana na virusi vya Covid-19 nchini Uhispania vimeendelea kuongezeka kwa idadi ya juu Jumanne wiki hii wakati mfumo wa afya nchini humo ukielemewa kwa kiasi kikubwa katika kutoa huduma kwa mamia kwa maelfu ya wagonjwa walioambukizwa.

Nchini Marekani, rais Donald Trump ameonya kuwa hali itakuwa mbaya zaidi ndani ya kipindi cha wiki mbili katika kupambana dhidi ya ugonjwa huo hatari, ambao umesababisha vifo vya watu zaidi ya 850 ndani ya masaa 24 nchini Marekani na ambapo mamlaka ya afya ina hofu kwamba idadi ya vifo itazidi 100,000 katika miezi michache ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.