Pata taarifa kuu
UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya visa nchini Ujerumani yaongezeka hadi 79,696

Watu 79,696 wameambukizwa virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19 ambao umesababisha vifo vya watu 1,017 nchini Ujerumani, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Ijumaa na taasisi ya Robert Koch (RKI) kwa magonjwa yanayoambukia.

Sars-CoV-2 ni virusi ambavyo husababisha ugonjwa wa Covid-19. Kuna walau chanjo 20 zinazotengenezwa kote duniani.
Sars-CoV-2 ni virusi ambavyo husababisha ugonjwa wa Covid-19. Kuna walau chanjo 20 zinazotengenezwa kote duniani. (Photo By BSIP/UIG Via Getty Images)
Matangazo ya kibiashara

Hii inaonyesha visa vipya 6,174 vya maambukizi na vifo vipya 145 kwa siku moja, kulingana na ripoti ya RKI.

Ugonjwa wa Covid-19 unaendelea kuathiri nchi mbalimbali duniani, huku maambukizi ya ugonjwa huo duniani yakifikia milioni moja, huku watu wakiendelea kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

Marekani inaendelea kuripoti visa vingi vya maambukizi ya virusi vya Corona, ambapo vifo vya watu 1,169 vimeripotiwa ndani ya masaa 24.

Wakati huo huo wanasayansi nchini Australia wameanza kufanya majaribio ya dawa mbili zinazoweza kuwa chanjo dhidi ya virusi vya corona.

Hiyo inatajwa kuwa ni "hatua muhimu " ya majaribio ya maabara.

Chanjo hizo zilizotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford na kampuni ya Marekani ya madawa - Inovio Pharmaceutical, zimeidhinishwa kufanyiwa majaribio kwa wanyama na Shrika la Afya Duniani (WHO).

Hata hivyo kuna chanjo nyingine kadhaa zinazofanyiwa uchunguzi katika maeneo mbali mbali duniani kwa sasa kwa kasi isiyo ya kawaida.

Lakini wanasayansi wa Jumuiya ya Madola wa Australia na Shirika la Utafiti wa kisayansi (CSIRO) wanasema vipimo vyao vitakuwa ni vya kwanza vilivyokamilika vya kutumia mnyama kabla ya kufanyika kwa vipimo halisi vya kliniki.

Idadi ya visa vya maambukizi vilivyothibitishwa ulimwenguni inazidi milioni moja leo Ijumaa, huku watu 52,000 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa Covid-19, kulingana na takwimu zilizotolewa na shirika la habari la AFP.

Ulaya ndio bara lililoathiriwa zaidi, lakini Marekani inaelekea kuwa kitovu kipya cha janga hilo, ikiripoti robo ya visa vya maambukizi. Idadi hii labda ni ndogo, kwa sababu ya ukosefu wa uchunguzi wa kutosha.

Nchini Marekani, idadi ya vifo katika masaa 24 imeiweka nchi hiyo kuwa na rekodi kubwa zaidi: vifo 1,169, kulingana na ripoti ya Chuo Kikuu cha Marekani cha Johns Hopkins.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.