Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Ubelgiji: Tuko tayari kumpa hifadhi ya ukimbizi Carles Puigdemont

Kiongozi wa jimbo la Catalonia nchini Uhispania Carles Puigdmont amekwenda nchini Ubelgiji. Hili limethibitishwa na wakili wake, wakati huu kukiwa na ripoti kuwa amekimbia nchi kwa hofu ya kukamatwa.

Kushoto, Carles Puigdemont, ambaye inasemekana kuwa alikimbilia uBelgiji kwa hofu ya kukamatwa.
Kushoto, Carles Puigdemont, ambaye inasemekana kuwa alikimbilia uBelgiji kwa hofu ya kukamatwa. REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya kiongozi huyo kuondolewa mamlaka ya kuongoza jimbo hilo baada ya wiki iliyopita, kutangaza uhuru wa jimbo hilo.

Mapema wiki hii Ubelgiji ilisema iko tayari kumpa hifadhi ya ukimbizi Carles Puigdemont.

Wanaharakati wa uhuru katika eneo la Catalonia wamekua wakiandamana ili eneo hiko liwe huru. Lakini Mwishoni mwa wiki iliyopita viongozi wa Uhispani walichukua uamuzi wa kufuta kujitenga kwa jimbo hulo na kuwa chini ya mamlaka ya serikali kuu ya Uhispania.

Hata hivyo viongozi wa Catalonia wameapa kuendelea na mchakato wao na kusema kuwa hawatotii kamwe serikali kuu ya Uhispania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.